Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mabosi Newcastle United wamfuata Isak nyumbani

ISAK Pict

Muktasari:

  • Isak amekuwa akihusishwa na mpango wa kuachana na maisha ya St James’ Park kwenye dirisha hili la majira ya kiangazi huku Liverpool ikitajwa kumsaka.

NEWCASTLE, ENGLAND: MABOSI wakubwa wa Newcastle United wamekutana na straika Alexander Isak kuweka mambo sawa ili staa huyo wa Sweden abaki.

Isak amekuwa akihusishwa na mpango wa kuachana na maisha ya St James’ Park kwenye dirisha hili la majira ya kiangazi huku Liverpool ikitajwa kumsaka.

Liverpool imeshashuhudia ofa ya Pauni 110 milioni kwa ajili ya Isak ikikataliwa, huku straika huyo akijiweka kando kwenye mazoezi za Newcastle. Msimamo wa Newcastle kuhusu kutokuwa na mpango wa kumuuza Isak bado haujabadilika, hivyo staa huyo hatakwenda kokote dirisha hili. Na sasa mabosi wa Newcastle wamechukua hatua ya mwisho katika mpango wa kumshawishi straika huyo abaki. Kinachoripotiwa ni kwamba mmiliki mwenza wa Newcastle, Jamie Reuben na jopo la maofisa wa PIF walimfuata Isak nyumbani kwake na kuzungumza naye ili abaki.

Reuben na mkurugenzi wa Newcastle, Jacobo Solis wote walikwenda kukutana na Isak nyumbani kwake huko Northumberland kabla ya mechi ya kichapoo kwa Newcastle mbele ya Liverpool huko St James’ Park.

Inaelezwa kwamba ishu ya mkataba mpya ilidaiwa kuwa sehemu kubwa ya mjadala huo na matumaini ni kwamba Isak atabaki. Alipoulizwa kuhusu mazungumzo hayo, kocha wa Newcastle, Eddie Howe alisema: “Sina ufahamu wa hilo, lakini sikuwa kwenye sehemu hiyo ya mazungumzo kwa muda mrefu.

“Hivyo, mimi nilikuwa na wajibu wa kuandaa timu, kuwahamasisha wachezaji wanaotaka kuichezea Newcastle.”

Mwenyekiti wa Newcastle United, Yasir Al-Rumayyan alikuwapo uwanjani St James’ Park, Jumatatu. Yeye hakuwa miongoni mwa waliokwenda kuzungumza na Isak, lakini anaamini straika huyo atabaki kikosini kwao.