Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Lukaku asikitishwa kushindwa kumzika Baba yake

Muktasari:

  • Rodger Lukaku (58), alifariki dunia Septemba 29 jijini Kinshasa, DR Congo ambako pia mazishi yake yamepangwa kufanyika huko.

Nyota wa Napoli, Romelu Lukaku amesema kuwa yeye na mdogo wake Jordan Lukaku watashindwa kumzika baba yao Roger Lukaku kwa vile wamezuiwa kuupeleka mwili wake Ubelgiji.

Rodger Lukaku (58), alifariki dunia Septemba 29 jijini Kinshasa, DR Congo ambako pia mazishi yake yamepangwa kufanyika huko.

Tangu alipofariki, Watoto wake, Jordan na Romelu wamekuwa wakipambana kupata idhini ya kuuzika mwili wa baba yao huko Ubelgiji ambako aliishi kwa muda mrefu kabla ya kurudi DR Congo ambako mauti yamemfika.

 Hata hivyo, hilo limeshindikana baada ya baadhi ya ndugu zao waliopo DR Congo kugoma na kutaka mwili wa Roger Lukaku kuzikwa ndani ya ardhi alikozaliwa.

“Baba yetu amefariki Septemba 28 na sisi kama ndugu tumejaribu kila kitu kuuleta mwili wake Ulaya lakini tunahisi kwamba tumekwamishwa na baadhi ya watu.

 “Kama baba yetu angekuwepo hapa leo, asingekubaliana na hili. Imevunja nyoyo zetu kwa kushindwa kumpumzisha baba yetu. Lakini ndugu hawakulitaka hilo.

“Tunafahamu sasa kwa nini baba yetu alituweka mbali na watu wengi,” — ameeleza Lukaku kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Baba wa Lukaku atazikwa ijumaa Oktoba 17, 2025 Kinshasa