Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Louis Van Gaal afunguka kupona tezi dume

VAN GAAL Pict

Muktasari:

  • Bosi huyo wa zamani wa Manchester United, Van Gaal, 73, amefunguka kuhusu kupona tezi dume baada ya kufanyiwa upasuaji mara kibao katika kipindi cha miaka ya karibuni.

AMSTERDAM, UHOLANZI: KOCHA Louis van Gaal amefichua ameshinda vita ya kumbana na maradhi ya saratani baada ya kudai sasa hana tena tezi dume.

Bosi huyo wa zamani wa Manchester United, Van Gaal, 73, amefunguka kuhusu kupona tezi dume baada ya kufanyiwa upasuaji mara kibao katika kipindi cha miaka ya karibuni.

Akizungumza katika kipindi cha televisheni cha Humberto, Van Gaal alisema: “Sasa hivi sisumbuliwi tena na saratani. Miaka miwili iliyopita, nilifanyiwa upasuaji mara kadhaa. Ilikuwa mbaya sana kipindi kile. Lakini, mwisho wa yote imelipa.”

Aliongeza: “Nafanya vipimo kila baada ya miezi michache na naendelea vizuri. Nakuwa fiti.”

Van Gaal alisema kwamba alikuwa akifanya siri tatizo lake hilo na kuwaficha wachezaji wa timu ya taifa ya Uholanzi kwa kuwa hakutaka kuathiri viwango vyao uwanjani wakati alipokuwa kocha na alisema: “Sikutaka kuwaambia wachezaji wangu kwa sababu sikutaka kuathiri viwango vyao. Katika kipindi nikiwa kocha wa timu ya taifa, nilikuwa naondoka usiku kwenda hospitali bila ya wachezaji kufahamu. Kipindi hicho nilikuwa nikidhani nipo na afya bora, kumbe haikuwa hivyo.”

Van Gaal alijiuzulu kuinoa timu ya taifa ya Uholanzi 2022 na tangu wakati huo amekuwa mshauri wa klabu ya Ajax, ambayo aliwahi kuinoa na kubeba taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya mwaka 1995.

Van Gaal amefanya mengi kama kocha akizinoa klabu kubwa kabisa kama Barcelona, Ajax, Bayern Munich na Man United na mara tatu tofauti alikuwa kocha wa timu ya taifa ya Uholanzi.

Ameshinda mataji makubwa kama Ligi ya Mabingwa Ulaya, Bundesliga, La Liga, Uefa Supercup na Eredivisie. Timu ambayo hakufanya mambo makubwa sana ni Man United, ambako alishinda tu Kombe la FA mwaka 2016, huku timu yake ikimaliza nafasi ya nne na tano kwenye msimamo wa Ligi Kuu England kabla ya kufutwa kazi na kibarua chake kukabidhiwa kwa Jose Mourinho.