Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Lookman anauzwa nje ya Italia

LOOKMAN Pict

Muktasari:

  • Fowadi huyo wa Kinigeria, Lookman, ambaye alifunga hat-trick kwenye fainali ya Europa League msimu uliopita, anajiandaa kwa ajili ya kwenda kukabiliana na changamoto mpya msimu ujao.

ROME, ITALIA: KLABU za Ligi Kuu England zitapigana vikumbo kuwania huduma ya mkali wa Atalanta, Ademola Lookman baada ya klabu yake kufichua itakuwa tayari kumpiga bei nje ya Italia dirisha lijalo.

Fowadi huyo wa Kinigeria, Lookman, ambaye alifunga hat-trick kwenye fainali ya Europa League msimu uliopita, anajiandaa kwa ajili ya kwenda kukabiliana na changamoto mpya msimu ujao.

Hilo limekuja baada ya Kocha wa Atalanta, Gian Piero Gasperini kudai Lookman ni mmoja ya waiga penalti wa ovyo zaidi kuwahi kuwaona kwenye mchezo wa soka baada ya mkali huyo kukosa mkwaju wake kwenye mechi ya kipigo cha mabao 3-1 kwenye mechi ya mchujo wa kutinga hatua ya mtoano kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Club Brugge.

Mmiliki mwenza wa Atalanta, Stephen Pagliuca tangu wakati huo amekuwa upande wa Lookman baada ya tofauti hiyo na kudai kocha Gasperini hakutoa maelezo yenye haki.

Pagliuca alisema: “Amefanya kosa kwa kumshambulia mtu binafsi. Hapa Atalanta, tunaishi kama familia na hiyo ndiyo sera yetu. Kama mambo hayaendi vizuri, basi tunawajibika kama kundi. Tunajitathmini na kutafuta namna ya kuboresha.”

Staa huyo wa zamani wa Everton, Fulham na Leicester City, Lookman alikaribia kuachana na Atalanta dirisha la majira ya kiangazi la mwaka jana wakati iliporipotiwa amefikia makubaliano binafsi na klabu ya soka ya Ufaransa, Paris Saint-Germain.

Hata hivyo, miamba hiyo ya Ufaransa ilishindwa kumnasa staa huyo na badala yake ilipofika Januari ilivamia huko Napoli na kumchukua Khvicha Kvaratskhelia. Juventus inamtaka Lookman, lakini Atalanta haitaki kuuza silaha kwa wapinzani wao wa ligi moja na badala yake ipo tayari kumuuza ng’ambo.

Arsenal na Liverpool zilionyesha dalili ya awali ya kumtaka Lookman, ambaye bei yake inaweza kuwa Pauni 50 milioni.