Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

LOCKRIDGE: Bingwa mara 2 wa dunia aliyeishia kuwa ombaomba

Ombaomba Pict
Ombaomba Pict

Muktasari:

  • Eneo hilo palikuwapo pia duka la uuzaji vyakula, lakini halikuwa linavutia watu ukilinganisha na dada aliyesimama barabarani ambaye alikuwa akiuza dawa ya levya hadharani. Alikuwa akipiga kelele "Dola tano, dola tano," kwa yeyote anayepita.

ROCKY Lockridge alikuwa akionekana juu ya kizingiti. Macho yake yalikuwa yakitazama vyema mandhari ya mitaa ya 7th Street na Chestnut huko Camden.

Eneo hilo palikuwapo pia duka la uuzaji vyakula, lakini halikuwa linavutia watu ukilinganisha na dada aliyesimama barabarani ambaye alikuwa akiuza dawa ya levya hadharani. Alikuwa akipiga kelele "Dola tano, dola tano," kwa yeyote anayepita.

Hiyo ndio ilikuwa mitaa ya bondia wa zamani wa Marekani, Rocky Lockridge, ambaye aliwahi kuwa bingwa wa dunia mara mbili.

Watu mbalimbali walionekana wakishuka kwenye magari yao na kwenda hadi pale alipokuwa amekaa Rocky, walikuwa wakimkumbatia na kuongea kisha baadaye walimuachia chochote kitu na kuondoka.

Mmoja wao alikuwa ni msichana mwenye umri wa miaka 20, aitwaye Laquicha Smith, ambaye alipoulizwa na chombo cha habari cha huko Camden alisema: "Huyu ni Rocky. Yeye ni bingwa, bado ana uwezo."

Wakati huo sura ya Rocky ilionekana kuwa imejawa makovu, mapengo pia yalitawala vyema katika kinywa chake, pia mkononi alikuwa ameshikilia mkongoja wa chuma ambao ulimsaidia kutembea kwa sababu alikumbwa na ugonjwa wa kiharusi uliomfanya kupooza sehemu ya mwili wake.

Vidole vyake vilikuwa vikitetemeka mara zote alipokuwa akinyanyua  sigara kuiweka mdomoni, sauti yake pia ilikuwa imekauka na ilikuwa ngumu kuisikia.

"Kila mtu ananibusu, anapiga kelele, 'Bingwa, Bingwa, Bingwa,'" anasema Lockridge. "Napata furaha kuwa karibu nao kwa sababu wanapitia mapambano, sawa na mimi."

Lockridge, ambaye alianza kupigana ngumi za kulipwa mwaka 1978 huko Totowa, Marekani katika siku zake za mwisho mwili wake ulikuwa umeinama akitembea, ndevu zake za rangi ya kijivu zilizomzunguka kidevuni zilimfanya aonekane mzee kuliko umri wake.

Alikiri kwamba ana tatizo la kutumia dawa za kulevya kwa zaidi ya miaka 20 "Ninakunywa na kutumia dawa kwa kiasi kikubwa," anasema na akafunguka kuwa hiyo ndio ilikuwa sababu yakuwa mbali ya mkewe na watoto wake.

"Niko na uchungu. Niko na uchungu mkubwa," alisema Rocky huku maneno yakitoka polepole na kwa kutetemeka. "Nimefanya makosa, makosa mengi,"

Haya ni kwa ufupi juu ya maisha ya bondia huyu Mmarekani Rick Lockridge maarufu kama  "Rocky" ambaye aliwahi kuwa bingwa wa super-featherweight akiutetea mara mbili kati ya mwaka 1984 hadi 1985.

Hadi anaachana na masumbwi alikuwa amepigana mapambano 53 akishinda 44 na kupoteza tisa.

Je nini kilimkuta hadi kufikia hatua hiyo kabla ya kufariki dunia mwaka 2019, hapa tumekuletea mkasa mzima wenye kusisimua.


OMBA01
OMBA01

ALIONEKANA KUWA TOFAUTI

Daima alionekana kuwa mtu mwerevu na mwenye kufikiria sana mambo kitaaluma. Alipokuwa na umri wa miaka 19 ambapo ndio rasmi alianza kupigana mapambano ya kulipwa nwaka 1978, Lockridge alikuwa chini ya usimamizi wa kampuni ya Main Events ambayo inamilikiwa na familia ya Duva, na mapigano yake ya mwanzo yalifanyika katika ukumbi wa Ice World.

Lockridge mmoja kati ya mabondia wachache ambao walifikiria maisha  baada ya masumbwi. Alisoma masomo ya biashara katika Chuo Kikuu cha William Paterson huko Wayne kwa miaka miwili.

Kathy Duva, ambaye sasa ni  Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Main Events na wakati huo alikuwa ni mtaalamu wa masuala ya umma kwenye kampuni hiyo anakiri kuwa Lockridge alikuwa tofauti.

"Rocky alikuwa mtu wa kawaida tu na  mwenye tabia njema," anasema. "Alikuwa mnyenyekevu, mwenye ufasaha katika mambo yake pia mtu mzuri."

Bondia huyu alipata umaarufu zaidi miaka ya 80 ambapo alishinda mapambano kadhaa ikiwemo lile dhidi ya Roger Mayweather( mjomba na mkufunzi wa bingwa wa bondia Floyd Mayweather Jr), aliyempiga kwa  knockout ya raundi ya kwanza ambapo alifanikiwa kushinda taji la WBA  Februari, 26,  1984.

Pambano lake dhidi ya Mayweather, ambalo lilidumu kwa sekunde 91, alipigana akiwa na umri wa miaka 25 na wakati huo alikuwa ameshashida mapambano 32 kati ya 35.

Baada ya hapo, walipata pesa za kutosha na yeye na mkewe, Carolyn, walihamia Mount Laurel, kitongoji cha kifahari cha Philadelphia huko South Jersey. Carolyn alijifungua mapacha Ricky na Lamar tarehe 23 Agosti, 1984.

Baada ya hapo alilitetea taji lake mara mbili kabla ya kupoteza mwaka 1985 kwa Wilfredo Gomez kisha akajaribu kulitetea mwaka 1986 kwa  Julio Cesar Chavez lakini akashindwa.

Alipata nafasi ya kushinda tena taji hili mwaka 1987 alipomchapa Barry Michae kutoka Uingereza.

Alilitetea tena mara mbili kabla ya kupoteza mbele ya Tony Lopez katika pambano la raundi 12 lililoitwa Pambano la Mwaka 1988 na jarida la Ring Magazine. Alipoteza pia pambano la marudiano la jasho na damu mwaka mmoja baadaye, kisha akastaafu baada ya ushindi mmoja wa mwisho mwaka 1989, dhidi ya Mike Zena


OMBA02
OMBA02

ALIVYOPOTEZA PESA ZAKE

Baada ya kila pambano, Lockridge anasema alikunywa "kwa wiki mbili." Alimeza cocaine na kutumia pombe, ambapo alikuwa akinywa yoyote ile iliyokuwa mbele yake.

Alipohitaji pesa, anasema angeenda kwa Duvas(waliokuwa wakimsimami) na wao wangeweza kumsaidia jambo ambalo analijutua na kufunguka kuwa hawakutakiwa kumpa pesa.

"Sikuwa na udhibiti wa kifedha, lakini masuala hayo hayakuwa na umuhimu kwangu kwa wakati huo. Nilitaka kuona watu walio karibu yangu wanafurahi namimi pia nina furahi,"alisimulia Lockridge.

Lockridge anasema pia hakuwa anapata pesa nyingi kama malipo ya mapambano yake jambo ambalo Kathy Duva alikuthibitisha akisema, bondia huyo hakupata pesa ambazo zingemfanya kuishi milele bila ya shida yoyote na pambano ambalo lilimpa pesa nyingi zaidi lilikuwa ni lile dhidi ya  Chavez, ambapo alipata Dola 200,000.

"Alikuwa na familia, watoto na alinunua nyumba," anasema Kathy Duva. "Pesa hupotea. Watu wanaotumia dawa za kulevya mara nyingi huishia katika shida kubwa. Ni aibu, lakini ni chaguo wanalochagua."

Baada ya kufeli katika mapambano mawili aliyojaribu kupigana baada ya kustaafu, mwaka 1992, Ricky alistaafu rasmi masumbwi.

Licha ya nia yake ya kutaka kurejea tena ulingoni, ilishindikana kwani miezi kadhaa baadae baada ya kutangaza kuachana na mchezo huo alipata ajali mbaya ya gari iliyosababisha apate jeraha la kichwa.

Ajali hiyo ambayo ilisababishwa na kuendesha akiwa amelewa pia ilichangia kumfanya aumwe kiharusi na tangu hapo hakuweza tena sio tu kupigana bali hata kuwa mwalimu wa mabondia wengine.

Hakuwa anaingiza chochote tena na kila siku zilivyozidi kwenda maisha yalikuwa magumu kwani familia ya watoto wawili aliyokuwa nayo ilihitaji huduma na pia kulikuwa na bili mbalimbali za kulipa., Je nini kitafuata?