Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Liverpool yarudi katika ubora wake ikiichapa Real Madrid

Muktasari:

  • Mabingwa hao wa England chini ya kocha Arne Slot, walimaliza kipindi kigumu cha kupoteza mechi sita kati ya saba kwa ushindi dhidi ya Aston Villa, Jumamosi iliyopita na mwendelezo wa mafanikio uliendelea huku Real Madrid wakizidiwa kila idara.

LIVERPOOL, ENGLAND: Liverpool imerudi katika kiwango chake cha juu ilipoitandika Real Madrid kwa mchezo wa kuvutia na kupata ushindi muhimu wa Ligi ya Mabingwa nyumbani kwenye uwanja wa Anfield usiku wa Novemba 4, 2025.

Mabingwa hao wa England chini ya kocha Arne Slot, walimaliza kipindi kigumu cha kupoteza mechi sita kati ya saba kwa ushindi dhidi ya Aston Villa, Jumamosi iliyopita na mwendelezo wa mafanikio uliendelea huku Real Madrid wakizidiwa kila idara.

Ushindi wa Liverpool ulikuwa wa kishindo zaidi ya matokeo yanavyoonyesha, huku Alexis Mac Allister akivunja ukimya katika kipindi cha pili, wakati Trent Alexander-Arnold, aliyekuwa beki wa zamani wa Liverpool, akitazama kutoka benchi huku timu yake mpya ikiwa haina makali.

Kipa wa Real Madrid, Thibaut Courtois, alifanya kazi kubwa kuzuia mabao kwa mashambulizi mfululizo, ikiwemo mikwaju minne kutoka kwa Dominik Szoboszlai na mpira wa kichwa wa Virgil van Dijk uliookolewa kwa ustadi wa hali ya juu.

Hata hivyo, Courtois hakuweza kuzuia bao la Liverpool, wakati Mac Allister alipotia kichwa mpira wa adhabu uliopigwa na Szoboszlai dakika ya 61.

Alexander-Arnold aliingia uwanjani dakika kumi za mwisho za mchezo, huku akizomewa na mashabiki wa Liverpool waliowahi kumshangilia kipindi anaitumikia klabu hiyo, lakini hakuweza kufanya lolote la maana. 

Wachezaji nyota wa Real, Jude Bellingham na Kylian Mbappe, walizimwa kabisa, na hawakuweza kuizuia timu ya Slot kupata alama tatu muhimu ikiwa nyumbani.