Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Liverpool imemnasa Wirtz kibabe sana

LIVERPOOL Pict

Muktasari:

  • Mambo yalikuwa moto. Picha lilikuwa hivi, wakati Wirtz anashuka na ndege binafsi huko Blackpool, Mei mwaka huu, wengi walidhani alikwenda kukutana na kocha Pep Guardiola kwa ajili ya kujiunga Manchester City.

LIVERPOOL, ENGLAND: LIVERPOOL imepambana vita kali kwenye mchakamchaka wa kunasa saini ya kiungo mshambuliaji wa Kijerumani, Florian Wirtz ikifikia makubaliano ya kumsajili kwa ada ya Pauni 116 milioni.

Mambo yalikuwa moto. Picha lilikuwa hivi, wakati Wirtz anashuka na ndege binafsi huko Blackpool, Mei mwaka huu, wengi walidhani alikwenda kukutana na kocha Pep Guardiola kwa ajili ya kujiunga Manchester City.

Kwa kipindi hicho, Liverpool haikuonekana kuwa siriazi kwenye kufukuzia saini yake. Bayern Munich nayo kwa kipindi hicho ilikuwa ikifukuzia huduma ya staa huyo. Jambo hilo liliifanya Liverpool kuamini kwamba inahitaji kupambana kwa nguvu zote kunasa saini ya staa huyo anayesakwa na vigogo kibao huko Ulaya.

Klabu zote hizo tatu zilifanya mazungumzo na Wirtz na familia yake, akiwamo baba ambaye ndiye wakala, Hans-Joachim Wirtz. Kumbe ile safari ya Blackpool, Wirtz na familia yake wana nyumba huko na hawakutaka kutumia uwanja mkubwa wa ndege ili kujificha. Man City ilijiweka kando kwa sababu iliona dau lake ni kubwa sana.

Bayern ilionyesha dhamira, lakini kocha Vincent Kompany hakumshawishi atakwenda kumtumia vipi kwenye kikosi chake na Wirtz mwenyewe alitaka changamoto mpya, hivyo Liverpool ilibaki kuwa chaguo pekee mezani.

Kingine kilichomvutia kwenda Liverpool ni baada ya miamba hiyo inayonolewa na Mdachi, Arne Slot, kumnasa staa mchezaji mwenzake wa zamani wa Leverkusen, Jeremie Frimpong.

Man City baada ya kuona Leverkusen inahitaji Pauni 127 milioni, iliona ni bora ikawasajili Tijjani Reijnders, Rayan Ait-Nouri, Marcus Bettinelli na Rayan Cherki badala ya Wirtz, ambaye iliamini dili lake linaweza kufikia hadi Pauni 250 milioni kama zitalipwa bonasi zote pamoja na mshahara.

Liverpool imekubali kumsajili staa huyo aliyechangia mabao 30 msimu uliopita kwa ada ya Pauni 116 milioni na uhamisho wake unaweza kukamiliki wiki ijayo, huku ikiwa bado haijafahamika kama dili la mchezaji huyo mmoja ukiweka kando ada yake litakuwa limeigharimu Liverpool kiasi gani cha pesa kuanzia kwenye mishahara na bonasi.