Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Lionel Messi ana tatizo moja

New Content Item (1)
New Content Item (1)

Muktasari:

  • Messi ambaye ni mshindi wa Ballon d’Or mara nane, ni miongoni mwa wachezaji bora kuwahi kutokea katika historia ya soka akiwa katika sahani moja na Cristiano Ronaldo.

MILAN, ITALIA: STAA wa Inter Miami na Argentina, Lionel Messi ameendelea kuteswa na udhaifu mmoja ambao yupo nao na kila siku anatamani umuondoke kabla hajastaafu kucheza soka.

Messi ambaye ni mshindi wa Ballon d’Or mara nane, ni miongoni mwa wachezaji bora kuwahi kutokea katika historia ya soka akiwa katika sahani moja na Cristiano Ronaldo.

Kwa sasa, nyota huyu ndio anashikilia rekodi yan kuwa mchezaji aliyeshinda mataji mengi zaidi (45), kwenye soka ikiwa pamoja na 12 ya Ligi Kuu, manne ya Ligi ya Mabingwa, Copa America mara mbili, na Kombe la Dunia moja.

Pia anashikilia rekodi nyingine kadhaa, zikiwamo za kuwa mfungaji bora wa Ligi ya Mabingwa Ulaya mara nyingi zaidi (mara sita), mabao mengi zaidi kwa timu moja (672 akiwa na Barcelona) pamoja na mabao mengi zaidi katika La Liga (474), hat-trick (36) na pasi za mabao (192).

Licha ya rekodi hizo, hadi leo Messi amekuwa akiwaambia watu wake wa karibu kwamba angetamani zaidi kuboresha zaidi uwezo wake wa kupiga penalti licha ya miaka minane kupita tangu aseme hadharani juu ya udhaifu wake huo.

“Je, kuna jambo moja ambalo linaniumiza, ningependa kuwa na ufanisi zaidi kwenye kupiga penalti. Kufanya mazoezi ya penalti si sawa na kuzipiga katika mchezo,” alisema Messi mwaka 2018 alipokuwa katika moja ya mahojiano.

Katika maisha yake ya soka la kulipwa, Messi amefunga jumla ya penalti 111, ikiwa ni pamoja na penalti aliyofunga katika mchezo wa fainali ya Kombe la Dunia dhidi ya Ufaransa. Hata hivyo, amekosa penalti 31, idadi sawa na mpinzani wake mkubwa Cristiano Ronaldo.

Mchezaji huyo wa Argentina amewahi kukosa penalti katika mechi muhimu kadhaa, ikiwa ni pamoja na nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa ya 2012 dhidi ya Chelsea, na fainali ya Copa America dhidi ya Chile.