Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Lamine Yamal aanza mazoezi binafsi

LAMINE Pict

Muktasari:

  • Yamal anatarajiwa kukosa mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi dhidi ya Cape Verde ili kumpa muda zaidi wa kuimarika.

Kiungo mshambuliaji Lamine Yamal, ameanza mazoezi binafsi ya uwanjani na gym. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 18 amekuwa nje ya uwanja kwa muda kutokana na majeraha yaliyomfanya akose mechi za mwisho za msimu wa ligi.

Hata hivyo, benchi la ufundi linachukua tahadhari kubwa ili kuzuia majeraha hayo kujirudia, ambapo amepangiwa ratiba ya kurejea uwanjani hatua kwa hatua.

Yamal anatarajiwa kukosa mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi dhidi ya Cape Verde ili kumpa muda zaidi wa kuimarika.

Mkakati uliopo ni kutumika kama mchezaji wa akiba kwenye mchezo wa pili dhidi ya Saudi Arabia, kabla ya kurejea rasmi kwenye kikosi cha kwanza akiwa fiti kwa asilimia mia moja kwenye mchezo wa tatu dhidi ya Uruguay.

LAMI 01

Lamine Yamal alikuwa anasumbuliwa na majeraha ya misuli ya paja la kushoto. Majeraha alioyapoata Aprili 22, 2026 wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Hispania (La Liga) dhidi ya Celta Vigo, ambapo aliumia baada ya kupiga mkwaju wa penalti.

Hatua ya kuanza mazoezi binafsi inaashiria maendeleo makubwa katika harakati zake za kurejesha utimamu wa mwili na kiwango chake cha ushindani kuelekea kombe la Dunia 2026.