Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kwa Arsenal Madrid ije tu

Muktasari:

  • Arsenal kwanza itakuwa na kibarua cha kucheza na PSV kwenye hatua ya 16 bora, ikipenya hapo itasubiri mshindi wa mchezo kati ya Real Madrid na Atletico Madrid.

LONDON, ENGLAND: MASHABIKI wa Arsenal wanaweza kuwa kwenye presha kubwa baada ya kufahamu kuna uwezekano wa kukwaruzana na Real Madrid kwenye robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya  - lakini wala hawapaswi kuogopa.

Arsenal kwanza itakuwa na kibarua cha kucheza na PSV kwenye hatua ya 16 bora, ikipenya hapo itasubiri mshindi wa mchezo kati ya Real Madrid na Atletico Madrid.

Lakini, kama Real Madrid ndiyo itakayokuja, basi Arsenal haipaswi kuwa na woga kutokana na rekodi zao.

Arsenal haijawahi kupoteza mbele ya Los Blancos, ambao wametinga 16 bora kwa kuitupa nje Manchester City. Arsenal na Real Madrid zimekutana mara mbili tu, mechi ya mtoano hatua ya 16 bora msimu wa 2005/6.

Shabiki mmoja alisema: “Ngoja kwanza, Real Madrid haijawahi kuifunga Arsenal? Hii imekaa poa.”

Kipindi hicho, Arsenal ya kocha Arsene Wenger iliweza kuidhibiti Real Madrid ile ya Galacticos, iliyokuwa na Ronaldo de Lima, Zinedine Zidane na David Beckham uwanjani na matokeo yalikuwa ya 0-0 kwenye mechi ya kwanza. Kwenye mechi ya pili, gwiji wa Arsenal, Thierry Henry alifanya maajabu, alipofunga bao la juhudi binafsi, alipopiga chenga wachezaji wanne wa Real Madrid na kumfunga kipa Iker Casillas kwa mguu wa kushoto. Arsenal ilifika fainali msimu huo, lakini ilichapwa na mahasimu wa Real Madrid, Barcelona 2-1.