Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kumbe Man United imemvutia waya Klopp

Muktasari:

  • Klopp alibwaga manyanga Liverpool majira ya kiangazi 2024 baada ya karibu miaka tisa ya kudumu Anfield, akisema anahitaji kupumzika ukocha.

MUNICH, UJERUMANI: NDO hivyo. Jurgen Klopp amekataa ofa kutoka Manchester United na pia angeweza kuwa kocha wa timu ya taifa ya England baada ya kuondoka kwa Gareth Southgate, anafichua wakala wake.

Klopp alibwaga manyanga Liverpool majira ya kiangazi 2024 baada ya karibu miaka tisa ya kudumu Anfield, akisema anahitaji kupumzika ukocha.

Tangu wakati huo, Mjerumani huyo amekuwa mkuu wa soka wa kimataifa katika kundi la Red Bull. Wakala wake wa muda mrefu, Marc Kosicke, alisema licha ya kupokea simu kutoka Man United na Chelsea, mteja wake hana mpango wa kurejea kufundisha kwa sasa.

Alipoulizwa kuhusu uwezekano wa Klopp kurejea kwenye benchi la ufundi, Kosicke alisema: “Kwa sasa sioni hilo likitokea, kwa sababu ana furaha sana katika nafasi yake mpya na mazingira haya. Labda siku moja atasema anahitaji kunusa harufu ya vyumba vya kubadilishia nguo tena. Lakini kwa sasa ana furaha sana katika jukumu lake.”

Kosicke aliongeza kuwa kabla ya kujiunga na Red Bull, Klopp angeweza kuifundisha timu ya taifa ya Marekani au England. Huenda pia angefundisha Ujerumani kama si uwepo wa Julian Nagelsmann.

“Chelsea na Man United pia waliulizia, ingawa Jurgen alikuwa ameshaweka wazi kwamba hatofundisha klabu nyingine yoyote nchini England. Maombi hayo hayajaacha kuja,” alisema Kosicke.

Hata hivyo, madai kwamba Chelsea waliwasiliana naye yamekanushwa na klabu hiyo ya Stamford Bridge. Katika mahojiano na Transfermarkt, Kosicke pia alidai kuwa Bayern Munich ilikaribia kumchukua Klopp mara mbili.

“Bayern walikaribia kumchukua mara mbili,” alisema na kuongeza. “Mara ya kwanza ilikuwa 2008: Uli Hoeness alimtaka Jurgen Klopp, lakini Karl-Heinz Rummenigge alimtaka Jurgen Klinsmann. Na baada ya Niko Kovac kuondolewa 2019, wakati Jurgen akiwa Liverpool, walitupigia tena. Hakuna aliyedhani mambo yangekuwa mazuri kiasi hicho chini ya Hansi Flick. Haikuwa muda sahihi.”