Kumbe Chelsea haina tiketi 2029
Muktasari:
- Lakini, Paris Saint-Germain timu ambayo ilifungwa na Chelsea kwenye mchezo wa fainali Jumapili iliyopita, yenyewe imeshakamatia tiketi hiyo ya kucheza fainali zijazo zitakazofanyika miaka minne ijayo. Chelsea iliichapa PSG mabao PSG 3-0 uwanjani MetLife na kunyakua taji hilo, shukrani kwa mabao matatu ya kipindi cha kwanza, yaliyofungwa na Cole Palmer mawili na Joao Pedro.
LONDON, ENGLAND: CHELSEA haijafuzu fainali zijazo za Kombe la Dunia la Klabu licha ya kushinda ubingwa wa michuano ya kwanza ya mashindano baada ya kufanyiwa mabadiliko.
Lakini, Paris Saint-Germain timu ambayo ilifungwa na Chelsea kwenye mchezo wa fainali Jumapili iliyopita, yenyewe imeshakamatia tiketi hiyo ya kucheza fainali zijazo zitakazofanyika miaka minne ijayo. Chelsea iliichapa PSG mabao PSG 3-0 uwanjani MetLife na kunyakua taji hilo, shukrani kwa mabao matatu ya kipindi cha kwanza, yaliyofungwa na Cole Palmer mawili na Joao Pedro.
Lakini, cha kushangaza, Chelsea haijakamatia tiketi ya kucheza Kombe la Dunia la Klabu 2029, licha ya kuwa mabingwa watetezi. Hiyo ni kwa sababu timu 32 zinazoshiriki fainali hizo tiketi zake zinagawiwa kwa mabara. Kwa utaratibu wa viwango vya Fifa, Uefa ina tiketi 12, CONMEBOL sita, AFC nne, CAF nne, CONCACAF nne, na OFC moja. Nchi mwenyeji itakayoandaa fainali hizo itakuwa na tiketi moja na hakuna tiketi yoyote kwa bingwa mtetezi, hivyo Chelsea ili kucheza Kombe la Dunia la Klabu la 2029 watapaswa kupambana kupata tiketi kwa kupitia zile 12 za Uefa.
Lakini, PSG yenyewe tayari imeshanyakua tiketi yake ya kucheza fainali zijazo ikiwa ni moja ya timu nne zitakazobeba ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya hadi kufikia kipindi hicho cha fainali.
Baada ya mabingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya kupata tiketi, nafasi nyingine zilizobaki kwa Uefa zitazingatia viwango vya ligi mbalimbali za Ulaya.
Na Chelsea kwa sasa inashika nafasi ya 14 kwenye viwango vya ubora, hivyo itapaswa kupambana kupanda juu au kushinda ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya hadi kufikia 2029.
Hata hivyo, Chelsea huenda haisikitiki sana juu ya kutokuwa na tiketi ya michuano ijayo kwa sasa, imeondoka kwenye fainali hizi za Marekani imeondoka na taji na mkwanja wa Pauni 97 milioni.