Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kuhusu Rashford  kucheza Barca ipo hivi

RASHFORD Pict

Muktasari:

  • Rashford, mwenye umri wa miaka 27, amejiunga na Barca kwa mkopo wa msimu mmoja kutoka Manchester United mapema mwezi huu na tayari ameshacheza mechi za kirafiki dhidi ya Vissel Kobe na Seoul.

BARCELONA, HISPANIA: STAA wa Manchester United, Marcus Rashford  ambaye amejiunga na Barcelona kwa mkopo wa msimu mmoja katika dirisha hili, amezungumza kwa mara ya kwanza kuhusu hofu kwamba huenda akashindwa kucheza La Liga msimu ujao itakaposhindikana kusajiliwa katika mfumo kutokana na sheria za matumizi ya pesa za ligi hiyo.

Rashford, mwenye umri wa miaka 27, amejiunga na Barca kwa mkopo wa msimu mmoja kutoka Manchester United mapema mwezi huu na tayari ameshacheza mechi za kirafiki dhidi ya Vissel Kobe na Seoul.

Mkataba huo wa mkopo unajumuisha pia chaguo la kununuliwa kwa Pauni 26 milioni msimu ujao kama klabu itavutiwa na kiwango chake.

Hata hivyo, kwa mujibu wa Barca Universal, taratibu za usajili wake rasmi kwa ajili ya msimu mpya wa La Liga bado hazijakamilika.

Tatizo hili linafanana na lililotokea msimu uliopita ambapo Barcelona iliweza kuwasajili Dani Olmo na Pau Victor baada ya msimu kuanza.

Kwa sasa, Rashford na kipa mpya Joan Garcia bado hawajasajiliwa rasmi. Lakini Rais wa klabu hiyo, Joan Laporta, amesema wazi kuwa shughuli za usajili bado hazijafungwa.

Akizungumza na MARCA Jumamosi, Laporta alisema: “Kama klabu, tunahitaji kuwa na wachezaji wengi zaidi ya kawaida. Hii inamaanisha tunawekeza zaidi, na tunapaswa kufanya kila jitihada kuwa na kikosi cha ushindani. Tuna wachezaji wenye vipaji vikubwa, lakini bado ni binadamu. Wanahitaji muda wa kupumzika na kufurahia maisha.”