Konate afichua siri ya Mbappe, Real Madrid
Muktasari:
- Mkataba wa Konate kwenye kikosi cha Liverpool utafika tamati mwishoni mwa msimu huu. Na kwa hali ilivyo, Konate hakuna uwezekano wa kusaini dili jipya la kuendelea kubaki Anfield, hivyo ataruhusiwa kuondoka mkataba wake utakapofika tamati mwakani.
PARIS, UFARANSA: BEKI wa kati wa Liverpool, Ibrahima Konate ametania kwamba Kylian Mbappe alikuwa akimpigia kila siku baada ya saa mbili baada ya kuripotiwa kwamba anajiandaa kwenda kujiunga na Real Madrid.
Mkataba wa Konate kwenye kikosi cha Liverpool utafika tamati mwishoni mwa msimu huu. Na kwa hali ilivyo, Konate hakuna uwezekano wa kusaini dili jipya la kuendelea kubaki Anfield, hivyo ataruhusiwa kuondoka mkataba wake utakapofika tamati mwakani.
Real Madrid imeripotiwa moja ya timu zinazopambana kunasa huduma ya beki huyo bure kabisa kwenye dirisha lijalo la majira ya kiangazi. Na Konate alijaribu kufunguka akidai alikuwa akizungumza na staa wa Real Madrid karibu kila siku.
Alipoulizwa kama Mbappe alijaribu kumshawishi aende Hispania, Konate alismea: “Alinipigia kila baada ya saa mbili.” Wakati huo huo, Koante aliulizwa kama anaweza kuzungumza Hispaniola, alijibu “hapana”.
Mbappe kwa upande mwingine alisema anaamini Liverpool itakuwa miongoni mwa timu zitakazoshindania mataji kwenye Ligi Kuu England msimu huu. Lakini, mkali huyo wa Los Blancos anaaini Arsenal na Manchester City zitakuwa kwenye mbio za ubingwa wa ligi hiyo.