Kombe la Dunia 2026, ombi la Iran lawekwa 'kapuni'
Muktasari:
- FIFA imesisitiza kuwa hakuna mpango wa kubadilisha ratiba rasmi iliyotangazwa Desemba 6, 2025.
Shirikisho la Soka Ulimwenguni (FIFA) limepiga chini ombi la Iran la kutaka kucheza mechi zake za Kombe la Dunia 2026 nchini Mexico badala ya maeneo yaliyopangwa awali.
FIFA imesisitiza kuwa hakuna mpango wa kubadilisha ratiba rasmi iliyotangazwa Desemba 6, 2025.
Msemaji wa FIFA ameiambia The Athletic kuwa wanatarajia timu zote kufuata ratiba kama ilivyopangwa.
Sababu kuu zilizofanya Iran iombe mabadiliko hayo kwa ajili ya Kombe la Dunia 2026:
Usalama wa Timu: Iran ina hofu na usalama wa wachezaji wake kutokana na uhusiano mbaya wa kisiasa kati yake na Marekani pamoja na Israel.
Kauli ya Trump: Rais Donald Trump alikaririwa akisema si 'sahihi' kwa Iran kucheza Marekani kwa ajili ya usalama wao wenyewe, jambo lililotafsiriwa kama tishio.
Changamoto za Visa: Balozi wa Iran nchini Mexico ameishutumu Marekani kwa kuweka vikwazo na kutoonyesha ushirikiano katika utoaji wa visa kwa msafara wa timu hiyo.
Hali ya Kivita: Mvutano wa kijeshi na mashambulizi ya anga yanayoendelea yamefanya Iran kuona safari ya Marekani kuwa ni hatari kubwa.