Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kocha wa Dubois afunguka siri ya kumpiga AJ

Muktasari:

  • Dubois alimpiga Joshua kwa KO katika raundi ya tano kwenye pambano lao lililofanyika London, England kwenye uwanja wa Wembley ambapo kulikuwa na mashabiki 98,000.

KOCHA wa bondia, Daniek Dubois amefichua kuwa moja kati ya vitu vilivyochangia bondia huyo kushinda pambano dhidi ya Anthony Joshua ulikuwa ni ujumbe wa maneno 16 aliompa kabla ya kupanda ulingoni.

Dubois alimpiga Joshua kwa KO katika raundi ya tano kwenye pambano lao lililofanyika London, England kwenye uwanja wa Wembley ambapo kulikuwa na mashabiki 98,000.

Kocha msaidizi wa Dubois,  Kieran Farrell amefunguka kwamba kabla ya kengele ya kuashiria pambano kuanza alimpa maneno ya hekima ambayo kwa kiasi kikubwa anaamini yalimsaidia kushinda pambano hilo kubwa.

“Kitu cha kwanza tulichomwambia Daniel ni ‘Nenda ukampe kitu ili ajue kuwa yuko ulingoni nawewe,’; ndivyo alivyoenda kufanya,” alisema Farrell alipozungumza na tovuti ya BoxingScene.

Dubois, ambaye amepigana mapambano 24, akishinda 22 (21 ikiwa ni kwa KO), alimwangusha Joshua mara tatu ikiwa ni katika raundi ya kwanza, ya tatu na yanne kabla ya kumwangusha raundi ya tano na kushinda.

Promota wa AJ,  Eddie Hearn amefichua kwamba uwezekano wa pambano hilo kurudiwa nchini Saudi Arabia upo na tayari mamlaka za soka nchini humo zimeshakubali.