Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kocha Spurs yupo matatani

SPURS Pict

Muktasari:

  • Kwa mujibu wa tovuti ya The Telegraph, Spurs inatarajiwa kufanya uamuzi wiki ijayo kuhusu hatma ya Postecoglou baada ya msimu uliomalizika kutofanya vizuri, wakimaliza nafasi ya 17 kwenye Ligi Kuu  England.

LONDON, ENGLAND: INAELEZWA nafasi ya kocha wa Tottenham, Ange Postecoglou, iko hatarini sana licha ya kuiwezesha timu hiyo kufuzu Ligi ya Mabingwa kwa kuchukua ubingwa wa Europa League.

Kwa mujibu wa tovuti ya The Telegraph, Spurs inatarajiwa kufanya uamuzi wiki ijayo kuhusu hatma ya Postecoglou baada ya msimu uliomalizika kutofanya vizuri, wakimaliza nafasi ya 17 kwenye Ligi Kuu  England.

Mwenyekiti wa timu hiyo, Daniel Levy amekuwa nje ya England tangu fainali hiyo ipigwe, huku Postecoglou akiwa likizoni, na uamuzi kuhusu hatma yake unatarajiwa kutolewa hivi karibuni na inaelezwa nafasi yake iko kwenye hatari kubwa sana.

Inasemekana Levy ana mpango wa kufanya mabadiliko ndani ya Spurs kwani hafurahishwi na jinsi ambavyo msimu uliomalizika ulivyokuwa ambapo walishinda mechi 11 tu na kupoteza 22.

Spurs inaripotiwa kuwa na nia ya kumchukua kocha wa Brentford, Thomas Frank na ikishindikana inaweza kuangukia kwa  kocha wa Fulham, Marco Silva, au Andoni Iraola kutoka Bournemouth.

Ingawa Postecoglou alimaliza ukame wa mataji wa miaka 17 kwa timu hiyo, inaonekana kuwa haitoshi kwa Levy ambaye amechukizwa na matokeo mabovu ya ligi.