Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kipigo kizito cha Vasco da Gama chamliza Neymar

NEYMAR Pict

Muktasari:

  • Mshambuliaji huyo,33, alirudi katika klabu hiyo aliyokuwa akiichezea utotoni, mwanzoni mwa mwaka huu baada ya kuishi na majeraha kwa kipindi cha takriban miezi 18 akiwa na Al-Hilal ya Saudi Arabia.

SANTOS, BRAZIL: STAA wa Santos, Neymar alionekana akilia kwa uchungu baada ya timu yake kupokea kichapo cha mabao 6-0 kutoka kwa Vasco da Gama wikiendi iliyopita.

Mshambuliaji huyo,33, alirudi katika klabu hiyo aliyokuwa akiichezea utotoni, mwanzoni mwa mwaka huu baada ya kuishi na majeraha kwa kipindi cha takriban miezi 18 akiwa na Al-Hilal ya Saudi Arabia.

Tangu arejee amefunga mabao sita na kutoa pasi tatu za mabao katika mechi 19 alizocheza akiwa na timu hiyo ambayo kwa sasa inashika nafasi ya 15 Ligi Kuu Brazil ikiwa ina tofauti ya pointi mbili tu dhidi ya timu zilizo kwenye nafasi ya kushuka daraja.

Kipigo cha mabao sita katika mchezo mmoja kilikuwa cha kwanza kwa Neymar katika maisha yake ya soka hali iliyosababisha ashindwe kujizuia na kuangua kilio akiwa uwanjani.

Neymar ambaye ililazimika kuondolewa uwanjani kwa msaada wa mmoja wa wafanyakazi wa benchi la ufundi wa klabu hiyo, kipigo chake kikubwa alichowahi kukipata katika maisha yake ya soka kilitokea Septemba 2015 wakati Barcelona ilipofungwa mabao 4-1 na Celta Vigo katika La Liga.

Baada ya kuonyesha hisia zake, Neymar alitoa maneno makali alipoulizwa juu ya kiwango cha timu yake.

"Najuta, nimevunjika moyo kabisa na utendaji wetu. Mashabiki wana haki ya kulalamika, wakiamua kutukana na kuonyesha hasira zao, watakuwa sahihi. Najisikia aibu sana. Sijawahi kupitia hili maishani mwangu. Kwa bahati mbaya leo limetokea. Machozi yangu yalitoka kwa hasira, kwa kila kitu. Kwa bahati mbaya, siwezi kupambana peke yangu kuisaidia timu. Kiukweli tulicheza vibaya sana na huo ndiyo ukweli."

Baada ya kipigo hicho kikali, Santos ilitoa taarifa ya kumfuta kazi kocha wao mkuu, Cleber Xavier ikiwa ni katika jitihada za kuinusuru timu.

Hivyo pia, Neymar, ambaye ndiye mfungaji bora wa muda wote wa timu ya taifa ya Brazil, awali alirudi Santos kwa mkataba wa muda mfupi Januari mwaka huu na alieleza lengo lake lilikuwa ni kucheza na kuonyesha kiwango bora kabla ya Kombe la Dunia la 2026. Baada ya mkataba huo wa muda mfupi aliongeza mwingine Juni mwaka huu ambao sasa utamalizika mwakani.