Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kipigo chaivuruga Liverpool

Muktasari:

  • Mechi hiyo iliyochezwa Villa Park ilishuhudia mashabiki wa Liverpool wakiondoka uwanjani kabla ya filimbi ya mwisho, hali iliyowakumbusha matokeo ya wikiendi iliyopita dhidi ya Chelsea ambapo hali kama hiyo ilitokea wakiwa nyumbani, Anfield.

LONDON, ENGLAND: JAHAZI la majogoo wa jiji Liverpool limejikuta likizama zaidi baada ya kupokea kichapo cha mabao 4-2 dhidi ya Aston Villa juzi, Ijumaa kilichoibua tena maswali mazito kuhusu ubora wa kikosi cha Arne Slot.

Mechi hiyo iliyochezwa Villa Park ilishuhudia mashabiki wa Liverpool wakiondoka uwanjani kabla ya filimbi ya mwisho, hali iliyowakumbusha matokeo ya wikiendi iliyopita dhidi ya Chelsea ambapo hali kama hiyo ilitokea wakiwa nyumbani, Anfield.

Dominik Szoboszlai ambaye amekuwa miongoni mwa wachezaji bora wa Liverpool msimu huu, alijikuta akiomba radhi kwa mashabiki wachache waliobaki baada ya kosa lake kuigharimu timu huku presha ikizidi kumlemea kocha Arne Slot.

Slot alikiri kabla ya mechi kuwa timu yake ilikuwa na majeruhi tisa, lakini alisisitiza kuwa hilo haliwezi kuwa kisingizio cha kiwango duni kilichoonyeshwa uwanjani.

Mchezaji wa zamani wa Liverpool Jamie Carragher alionya kabla ya mchezo akisema timu hiyo haichezi vizuri inapokuwa na mpira wala bila mpira, kauli iliyodhihirika tena dhidi ya Villa.

Kichapo hicho kimeifanya Liverpool kufikisha mechi 19 za kufungwa katika mashindano yote msimu huu huku rekodi yao ya ugenini dhidi ya timu za juu ikizidi kuwa mbaya, mechi 8, kupoteza 7 na sare 1.

Kocha Slot alisema: “Tumefungwa mabao mengi mno, tulikuwa bado ndani ya mchezo lakini baada ya bao la pili tulisambaratika.”

Katika mchezo huo, Liverpool ilionekana kukosa ubunifu na makali katika safu yao ya ushambuliaji, isipokuwa mchango wa kijana Rio Ngumoha mwenye umri wa miaka 17 ulionekana kwa kupiga mashuti machache.

Villa walitumia nafasi zao vizuri kupitia Ollie Watkins ambaye alifunga mabao mawili katika kipindi cha pili kilichojaa makosa ya mengi ya kujilinda kwa Liverpool.

Matokeo hayo yameiacha Liverpool katika hatari kuzidiwa kete na Bournemouth na Brighton katika mbio za kufuzu Ligi ya Mabingwa huku presha ikizidi kuelekea katika mchezo wao wa mwisho wa msimu dhidi ya Brentford.

Brighton na Bournemouth bado wana nafasi ya kubadili msimamo iwapo watafanya vizuri katika mechi zao zilizosalia, jambo linaloweza kuifanya Liverpool ipoteze nafasi hiyo.