Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kipa Donnarumma awaibua mashabiki

KIPA Pict

Muktasari:

  • Donnarumma aliwekwa kando kwenye kikosi cha PSG kilichocheza mechi ya Super Cup usiku wa Jumatano, ikiwa ni miezi michache imepita tangu alipoipa timu hiyo taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya.

PARIS, UFARANSA: MASHABIKI wa soka wameishambulia Paris Saint-Germain wakidai wamefanya uhalifu mkubwa kwa kumpiga chini kipa Gianluigi Donnarumma na kumpanga Lucas Chevalier ambaye alifanya makosa ya kizembe kwenye mechi yake ya kwanza katika kikosi hicho dhidi ya Tottenham.

Donnarumma aliwekwa kando kwenye kikosi cha PSG kilichocheza mechi ya Super Cup usiku wa Jumatano, ikiwa ni miezi michache imepita tangu alipoipa timu hiyo taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Kipa huyo Mtaliano aliwekwa kando na kocha Luis Enrique akidai sasa anafikiria mipango mingine. Wakala wa Donnarumma, Enzo Raiola, ametishia kuifungulia mashtaka PSG kutokana na walichomfanyia mteja wake.

Bila shaka, kipa huyo na wakala wake wote walikuwa na furaha baada ya kuona Chevalier akifanya makosa kwa kuruhusu Spurs kufunga mara mbili. Kosa la kwanza lilitokea baada ya kipa huyo mpya wa PSG kupangua mpira ambao ulikwenda kwa Micky van de Ven na kumalizia nyavuni.

Bao la pili lilitokea kwa makosa ya kipa Chevalier kwa kushindwa kudaka mpira wa Cristian Romero na hivyo kuusukumia nyavuni.

Jambo hilo liliwaibua mashabiki wa soka kwenye mtandao wa kijamii na kumtetea Donnarumma, ambaye anahesabika kama mmoja wa makipa bora.

Shabiki wa kwanza alisema: “Kumwondoa Donnarumma kwa ajili ya Chevalier ni kosa la jinai!” Mwingine alisema: “Huu ni uamuzi wa hovyo kabisa kumshusha thamani Donnarumma.”

Kuna shabiki alisema: “Ni kitu kizuri PSG imesajili kipa mzuri miguuni.”

Bahati nzuri kwa Chevalier ni alimaliza mechi hiyo kwa kicheko baada ya timu yake kushinda kwa mikwaju ya penalti na kunyakua ubingwa.

Licha ya PSG kuwa nyuma 2-0 hadi kwenye dakika tano za mwisho, ilipambana na kufunga mara mbili kupitia kwa Kang-In Lee na Goncalo Ramos kabla ya kushinda kwa mikwaju ya penalti 4-3. Spurs ilikosa penalti mbili na moja ya Van de Ven iliokolewa na kipa Chevalier, hivyo PSG ikabeba taji kibabe.