Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Joe Cole karata yake kwa Wirtz

COLE Pict

Muktasari:

  • Joe Cole, aliyewahi kuichezea Chelsea pia kwenye Ligi Kuu England, alisema soka la kisasa limekuwa tofauti kabisa na kuwapa wachezaji wa kigeni fursa nuzri ya kutamba.

LIVERPOOL, ENGLAND: STAA wa zamani wa Liverpool, Joe Cole amesema haamini Florian Wirtz hawezi kushindwa kutamba kwenye Ligi Kuu England kwa sababu tu amesajiliwa kwa pesa nyingi kwamba itamfanya kuwa na presha.

Joe Cole, aliyewahi kuichezea Chelsea pia kwenye Ligi Kuu England, alisema soka la kisasa limekuwa tofauti kabisa na kuwapa wachezaji wa kigeni fursa nuzri ya kutamba.

Wirtz, 22, atacheza mechi yake ya kwanza ya Ligi Kuu England ilifanyika usiku wa jana huko Anfield, wakati Liverpool ilipokipiga na Bournemouth baada ya uhamisho wake wa Pauni 116 milioni kutoka Bayer Leverkusen kwenye dirisha hili la majira ya kiangazi.

Cole alitabiri staa huyo mpya wa Liverpool atakwenda kutamba, aliposema: “Nadhani ya kutumia nguvu nyingi ni kitu kilichokuwa kikisemwa zamani, lakini si sasa. Kwa sasa, hilo si tatizo kabisa, lilikuwa nyuma huko.

“Kipindi kile hata wale wenye miili mikubwa kama Didier (Drogba) walipata shida. Sasa ni tofauti na nadhani, Wirtz, usajili wake wa pesa nyingi, hauwezi kumfanya awe na presha na kushindwa kufanya vizuri Ligi Kuu England.”

Cole anaamini mashabiki wa Liverpool si tu watafurahia kutazama ufundi wa kiungo Wirtz anapokuwa na mpira na kwenye kushambulia, bali pia watapata faida ya uwepo wake kwenye kikosi katika kunyang’anya mipira itapokuwa kwa wapinzani. Staa Wirtz amekuwa na kiwango bora kwenye kufunga mabao na kuasisti kitu ambacho kitakuwa na umuhimu mkubwa kwa kocha Arne Slot.