Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Jobe Bellingham kufuata nyayo za kaka yake

JOBE Pict

Muktasari:

Vyanzo kutoka timu hiyo ya Bundesliga vinasema kijana huyo mwenye umri wa miaka 19 ameahidi kujiunga baada ya kufanya mazungumzo na mkurugenzi wa michezo, Sebastian Kehl huko Ibiza wiki iliyopita.

DORTMUND, UJERUMANI: MABOSI wa Borussia Dortmund wana imani kuwa wameshinda mbio za kumsajili kiungo wa kati wa Sunderland, Jobe Bellingham ambaye ni mdogo wake Jude Bellingham anayekipiga Real Madrid.

Vyanzo kutoka timu hiyo ya Bundesliga vinasema kijana huyo mwenye umri wa miaka 19 ameahidi kujiunga baada ya kufanya mazungumzo na mkurugenzi wa michezo, Sebastian Kehl huko Ibiza wiki iliyopita.

Ada ya uhamisho inatarajiwa kuwa karibu Pauni 25 milioni, huku klabu yake ya awali, Birmingham City ikitarajiwa kupata mgawo wa asilimia 15.

Bellingham alikutana na Eintracht Frankfurt wiki iliyopita na pia alizungumza na RB Leipzig.

Hata hivyo, Dortmund inaamini ndio washindi kwenye hilo kwani wana ushawishi wa kumuonyesha njia ambayo kaka yake amepitia.

Jobe aliisaidia Sunderland kupanda daraja kwenda  Ligi Kuu England  mwezi uliopita, lakini alikuwa na nia ya kuhamia Bundesliga kwa ajili ya hatua inayofuata ya maendeleo ya maisha yake ya soka.

Jude anadaiwa kuwa pia anatumika kumshawishi mdogo wake ajiunge na Dortmund akimwelezea faida atakazopata na jinsi alivyonufaika na timu hiyo.

Borussia Dortmund ilimaliza ikiwa katika nafasi ya nne kwenye msimamo wa Bundesliga msimu huu na kupata nafasi ya kushiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao. Pia itashiriki katika Kombe la Dunia la Klabu la Fifa lililofanyiwa maboresho ambalo linatarajiwa kuanza Juni 15 nchini Marekani.

Dortmund iko katika Kundi F pamoja na Fluminense, Ulsan na Mamelodi Sundowns.