Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Jeremy Doku aenda kubatizwa fasta

DOKU Pict

Muktasari:

  • Winga huyo wa Kibelgiji alicheza kwa kiwango cha kibabe sana katika mechi hiyo na Man City iliibuka na ushindi wa mabao 3-0.

MANCHESTER, ENGLAND: STAA wa Manchester City, Jeremy Doku amekamilisha furaha yake ya kuwakanda Manchester United huko Etihad kwa kwenda kupatizwa na kumpokea Yesu.

Winga huyo wa Kibelgiji alicheza kwa kiwango cha kibabe sana katika mechi hiyo na Man City iliibuka na ushindi wa mabao 3-0.

Katika mechi hiyo, Doku alitengeneza mabao mawili ya kwanza, yaliyofungwa na Phil Foden na Erling Haaland na hakika alikuwa mwiba mchungu kwa mabeki wa Man United.

Baada ya mechi hiyo, Doku alikwenda kufanya tukio la ubatizo huku mwenyewe akibainisha amefanya hivyo kujiongoa kwenye dhambi.

Kabla ya kwenda kanisani, Doku alisema: “Kama nitakuwa mkweli, hii kitu kwangu ilikuwa ushindi wa mapema. Kwa nini? Kwa sababu nilijua baada ya mechi nakwenda kubatizwa.

“Pengine hilo ndiyo maana niliona kama nasukumwa hivi. Ndiyo maana nina furaha kutokana na kiwango changu pia.”

Doku, 23, alishasema kuhusu imani yake ya dini ilivyo kwenye maisha yake.

Kwenye hilo alisema: “Ni wazi, hii ndiyo maana ya maisha yangu. Hakuna kitu muhimu kwangu kuzidi imani yangu. Nikiwa kama Mkristo, unapobatizwa, utaachana na mambo ya zamani, dhambi zako za zamani zinakwisha, unaanza upya kuishi na Mungu. Unajirudisha kwa Mungu na Yesu Kristo.”

Wengi kubatizwa na familia zao wanapokuwa na umri mdogo, lakini Doku alisubiri jambo hilo na kulifanya ukubwani.