Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Jadon Sancho kuna tatu mezani

SANCHO Pict

Muktasari:

  • Winga huyo wa zamani wa Borussia Dortmund amerejea Man United baada ya Chelsea kukataa kumsainisha mkataba wa kudumu licha ya kuonyesha kiwango bora na kutumika katika mechi nyingi.

MANCHESTER, ENGLAND: WAKATI hatma yake ikiwa haijulikani hadi sasa, ripoti zinaeleza kuwa timu tatu za Ligi Kuu England zinainyemelea huduma ya winga Jadon Sancho wa Manchester United.

Winga huyo wa zamani wa Borussia Dortmund amerejea Man United baada ya Chelsea kukataa kumsainisha mkataba wa kudumu licha ya kuonyesha kiwango bora na kutumika katika mechi nyingi.

Licha ya kurejea, kocha Ruben Amorim anadaiwa kuwa wazi kabisa hana mpango wa kumrudisha  Sancho katika kikosi cha kwanza, jambo linalosababisha afikirie sehemu nyingine atakayocheza msimu ujao.

Kwa mujibu wa tovuti ya The Sun timu tatu ambazo ni Aston Villa, Tottenham na Newcastle zote zinafuatilia maendeleo yake.

Villa inatajwa kuwa na nia ya kumsajili kwa mkopo, lakini Man United inataka dili la fedha taslimu ili kuzitumia katika usajili wak kujenga kikosi upya.

Newcastle na Tottenham zote zinamwona Sancho kama chaguo lake la kwanza katika dirisha hili ambapo zinajenga vikosi vitakavyoziwezesha  kushindana katika Ligi Kuu na Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Borussia Dortmund pia ilikuwa ikimfuatilia Sancho, lakini imeacha naye baada ya  kumsajili Jobe Bellingham.

Licha ya kufunga katika ushindi wa mabao 4-1 wa fainali ya Europa Conference League dhidi ya Real Betis, Sancho hakuweza kukamilisha usajili wa Pauni 25 milioni kwenda Chelsea.

Chelsea awali ilimchukua Sancho kwa mkopo kutoka Man United na walikubaliana kumnunua kwa Pauni 25 milioni, ikiwa ingemaliza nafasi 14 za juu na ikiwa isingetaka kumnunua walitakiwa kulipa faini ya Pauni 5 milioni.

Baada ya Chelsea kumaliza nafasi ya nne na kutwaa taji la Conference League, iliamua kulipa adhabu ya hiyo Pauni 5 milioni badala ya kumchukua moja kwa moja.

Sasa, macho ya Chelsea yameelekezwa kwa mawinga wengine, akiwemo Jamie Byroe-Gittens wa Borussia Dortmund na Nico Williams wa Athletic Bilbao.

Vilevile  inahusishwa pia na Alejandro Garnacho, ambaye pa ameonyeshwa mlango wa kutokea kama ilivyokuwa kwa Sancho.