Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ishu ya Rudiger yafanyiwa kazi

RUDIGAR Pict

Muktasari:

  • Rudiger aliingia kwenye mechi hizo dakika za mwisho kuchukua nafasi ya Trent Alexander-Arnold katika kipute hicho kilichofanyika uwanjani Bank of America huko Charlotte.

CHARLOTTE, MAREKANI: SHIRIKISHO la kimataifa la vyama vya soka (FIFA) limeanzisha uchunguzi juu ya madai ya beki wa Real Madrid, Antonio Rudiger kufanyiwa ubaguzi wa rangi kwenye mechi ya fainali za Kombe la Dunia la Klabu dhidi ya Pachua iliyofanyika Jumapili usiku.

Rudiger aliingia kwenye mechi hizo dakika za mwisho kuchukua nafasi ya Trent Alexander-Arnold katika kipute hicho kilichofanyika uwanjani Bank of America huko Charlotte.

Wakati Rudiger anaingizwa tayari Real Madrid ilikuwa mbele ya mabao matatu. Los Blancos ilicheza mechi hiyo ikiwa pungufu baada ya beki wa kati, Raul Asencio, kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya saba tu.

Lakini, miamba hiyo inayonolewa na Xabi Alonso ikiwa 10 uwanjani, ilifunga bao dakika 10 kabla ya mapumziko kupitia kwa kiungo Jude Bellingham. Kisha Arda Guler aliongeza bao jingine kabla ya Federico Valverde kufunga la tatu zikiwa zimebaki dakika 20 mechi kumalizika. Wapinzani wao hao wa Mexico walifunga bao lao kupitia kwa Elias Montiel, dakika mbili baada ya Rudiger kuingia.

Kwenye dakika za majeruhi, Rudiger alitibuana na nahodha wa Pachuca, Gustavo Cabral. Baada ya kuzungumza na wachezaji hao, mwamuzi Ramon Abatti alionyesha ishara ya kufunga mikono yake kwa alama ya mkasi kifuani, akiwa na maana kuna kanuni ya ubaguzi imebunjwa.

Kinachoelezwa ni Cabral alidaiwa kutoa kauli ya kibaguzi dhidi ya Rudiger. Cabral alikanusha.

Rudiger alionekana kusisitiza jambo alipokuwa akizungumza na mwamuzi Abatti juu ya yale aliyoambiwa na Cabral. Kocha wa Madrid, Alonso alithibitisha Rudiger kutoa malalamiko ya kubaguliwa.

“Hicho ndicho alichozungumza Rudiger na tunamwaamini,” alisema Alonso.

Cabral aliendelea kukana kutoa lugha ya kibaguzi na kudai kwamba alichomwambia Rudiger ni maneno  ‘coward’ kwa maana ya kuwa mwoga kwa tafsiri ya Kiswahili.

Kocha wa Pachuca, Jaime Lozano alisema tena kwa kusisitiza hakuna mchezaji yeyote kwenye kikosi chake anayeweza kuwa mbaguzi.