Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Isak kuwekewa ngumu Newcastle

Muktasari:

  • Straika huyo wa kimataifa wa Sweden, mwenye umri wa miaka 25, alikosa ziara ya mechi za pre-season huko Asia na amekuwa akiwindwa na Liverpool.

NEWCASTLE, ENGLAND: KOCHA wa Newcastle United, Eddie Howe amesema straika Alexander Isak atapaswa kupambana kwelikweli kurudi kwenye mazoezi ya kikosi cha kwanza.

Straika huyo wa kimataifa wa Sweden, mwenye umri wa miaka 25, alikosa ziara ya mechi za pre-season huko Asia na amekuwa akiwindwa na Liverpool.

Newcastle ilielezea kukosekana kwa Isak kuwa ana majeraha madogo. Baadaye, zikaibuka taarifa kwamba straika huyo anataka kuondoka St James' Park.

Na staa huyo ameanza kufanya mazoezi kivyake huko kwenye klabu yake ya zamani ya Real Sociedad, lakini iliaminika amerudi Tyneside wikiendi iliyopita baada ya Liverpool kupeleka ofa ya Pauni 110 milioni, ambayo ilikataliwa.

Fowadi huyo hakujihusisha kwenye mazoezi na wenzake tangu alipoambiwa kurudi nyumbani kutoka Glasgow, wakati Newcastle ilipokipiga na Celtic, Julai 19, baada ya kuibuka kwa ishu ya uhamisho.

Baada ya sare ya bao 1-1 dhidi ya Tottenham huko Korea Kusini, kocha Howe aliulizwa kama Isak atarejea kwenye mazoezi ya kikosi cha kwanza wiki ijayo.

Bosi huyo wa Magpies alisema: "Atapaswa apambane kupata hiyo haki ya kufanya mazoezi na sisi. Sisi ni Newcastle United. Mchezaji anawajibika kuwa hapa, kuwa sehemu ya hii timu, hivyo ajitue kama anapaswa kucheza hapa.

"Tutahakikisha kwamba mchezaji anapaswa kupambana kushinda hiyo haki ya kufanya mazoezi na wenzake. Mchezaji hawezi kufanya vitu visivyoeleweka kisha akapata nafasi ya kufanya mazoezi na kikosi cha kwanza kikawaida tu."

Ripoti zinafichua kwamba Liverpool itarejea na ofa yake ya pili kwa ajili ya kumsajili Isak itakapoona Newcastle imepata mbadala wake.

Newcastle ipo kwenye vita kali na Manchester United kuwania saini ya straika wa RB Leipzig, Benjamin Sesko, ambapo imepeleka ofa ya Pauni 70 milioni kwa ajili ya kunasa huduma ya staa huyo wa kimataifa wa Slovenia.

Kocha Howe, 47, alisema hakuzungumza kitu chochote na Isak alipokuwa Asia.


MAVITU YA ISAK HUKO NEWCASTLE EPL 2024-2025

-Amecheza: Mechi 34

-Ametengeneza: Nafasi 42

-Amefunga: Mabao 23

-Ametoa: Asisti 6

-Amelenga golini: Mashuti 46

-Amepiga: Pasi 658