Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Isak awekewa ulinzi mkali Liverpool

ISAK Pict

Muktasari:

  • Fowadi huyo alikamilisha uhamisho wake wa Pauni 130 milioni kwenda Anfield katika siku ya mwisho ya kufungwa kwa dirisha la usajili wa majira ya kiangazi akitokea Newcastle United.

LIVERPOOL, ENGLAND: HALI ya afya ya straika ghali zaidi kwenye Ligi Kuu England, Alexander Isak itafuatiliwa kwa karibu zaidi na klabu yake mpya ya Liverpool wakati atakapokuwa kwenye majukumu ya timu ya taifa ya Sweden.

Fowadi huyo alikamilisha uhamisho wake wa Pauni 130 milioni kwenda Anfield katika siku ya mwisho ya kufungwa kwa dirisha la usajili wa majira ya kiangazi akitokea Newcastle United.

Baada ya kusaini mkataba, Isak haraka alisafiri kwenda Sweden kujiunga na timu ya taifa kwa ajili ya mechi za kimataifa, kufuzu Kombe la Dunia na timu hiyo itakipiga na Slovenia na Kosovo. Bado haijulikani Isak atakwenda kucheza huko kwenye kikosi cha Sweden baada ya staa huyo kufanya mazoezi kivyake kwa muda wote aliokuwa akivimbiana na Newcastle juu ya kulazimisha uhamisho wa kwenda Liverpool.

Isak, ambaye amefunga mabao 16 katika mechi 52 alizochezea Sweden, hana utimamu mzuri wa mechi kwa saabu hajacheza mechi yoyote ya kiushindani tangu alipofanya hivyo kwenye mechi ya mwisho ya Ligi Kuu England msimu uliopita. Sasa, Liverpool imeanza kuwa na wasiwasi juu ya usalama wa staa wao huyo, ambaye imemsajili kwa ada iliyovunja rekodi ya uhamisho Uingereza.

Kocha wa Sweden, Jon Dahl Tomasson alisema straika wake huyo amekuwa na furaha baada ya kujiunga na wenzake kwenye timu ya taifa. Fowadi huyo wa zamani wa AC Milan amekuwa akiwasiliana na Kocha Arne Slot wa Liverpool kwamba jopo la madaktari wa timu hizo mbili, wamejadiliana namna bora ya matumizi ya mchezaji Isak.

“Hatutafanya kitu chochote cha kijiunga kuhusu Isak,” alisema Tomasson.

“Hakuwa na pre-season wala kufanya mazoezi mengi na mechi. Hawezi kucheza dakika 90. Tuna mpango wetu. Amekuwa akitabasamu muda wote hapa kambini.

"Nilipoanza kazi, kulikuwa na kelele nyingi kuhusu Alexander Isak na Viktor Gyokeres kwamba hawawezi kucheza pamoja. Ninachoweza kusema, wanaweza."