Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Hebu sikieni kocha Amorim anachosema

Muktasari:

  • Kocha huyo Mreno alisema kwamba alikuwa tayari kurusha taulo baada ya udhalilishaji aliokumbana nao kwenye mechi ya kipigo kutoka kwa timu ndogo ya Grimsby Town na kutupwa nje ya michuano ya Kombe la Ligi.

MANCHESTER, ENGLAND: KOCHA wa Manchester United, Ruben Amorim amekiri kwamba hafahamu kama ataendelea kuwa kocha wa timu hiyo, lakini mwenyewe amesisitiza hana mpango wa kung’atuka.

Kocha huyo Mreno alisema kwamba alikuwa tayari kurusha taulo baada ya udhalilishaji aliokumbana nao kwenye mechi ya kipigo kutoka kwa timu ndogo ya Grimsby Town na kutupwa nje ya michuano ya Kombe la Ligi.

Kocha huyo alisema hisia kali zilimwandama sana katika mechi hiyo ambapo timu yake ilikutana na matokeo ya kushangaza zaidi katika historia yao. Na kinachoelezwa atakuwa na kikao kizito na mabosi wakubwa wa Man United wiki ijayo wakati wa mapumziko ya mechi za kimataifa.

Kocha wa zamani wa England, Gareth Southgate ni miongoni mwa makocha wanaopewa nafasi kubwa ya kwenda kuinoa Man United endapo Amorim atafutwa kazi, huku makocha wengine, Jose Mourinho na Ole Gunnar Solskjaer waliowahi kuinoa timu hiyo wakiwa hawana kazi kwa sasa.

Alipoulizwa kama ataendelea kuwa kocha wa timu hiyo endapo timu itakuwa imepoteza mbele ya Burnley katika mchezo wa Ligi Kuu England, uliopaswa kufanyika mchana wa Jumamosi, Amorim alisema: “Sifahamu nini kitatokea. Siwezi kutoa ahadi ya chochote ya kile kinachoweza kwenda kutokea. Mimi ni kocha wa Man United na nadhani hilo halitabadilika.”€

Baada ya mechi ya Burnley uwanjani Old Trafford, kikosi hicho cha Amorim kitakuwa na kasheshe la kucheza na Manchester City uwanjani Etihad na baadaye Chelsea.

Alipozungumzwa na waandishi huko Carrington, Amorim alisema kuna nyakati kabisa zilimfanya afikirie kung’atuka, aliposema: “Wakati mwingine nawachukia wachezaji wangu, wakati mwingine nawapenda na wakati mwingine nawatetea wachezaji wangu. Wakati mwingine nataka kung’atuka, wakati mwingine nataka kuwa hapa kwa miaka 20 ijayo.”€

Lakini, kubwa zaidi kocha huyo wa zamani wa Sporting Lisbon alisema hawezi kubadili staili yake ya uchezaji.