Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Halaand awajia juu wenzake kambini

Muktasari:

  • Man City imepoteza mechi mbili kati ya tatu za mwanzo ilizocheza kwenye ligi msimu huu na hivyo kushika nafasi ya 13 kwenye msimamo wa Ligi Kuu England.

MANCHESTER, ENGLAND: STRAIKA, Erling Haaland amewajia juu wachezaji wenzake wa Manchester City baada ya kuanza vibaya msimu wa Ligi Kuu England 2025/26 na kuwataka kukazama msuli dhidi ya Manchester United, leo Jumapili.

Man City imepoteza mechi mbili kati ya tatu za mwanzo ilizocheza kwenye ligi msimu huu na hivyo kushika nafasi ya 13 kwenye msimamo wa Ligi Kuu England.

Kwenye mechi iliyopita, ilipoteza uongozi wao wa 1-0 na kuchapwa 2-1 na Brighton baada ya kutokea kwenye mechi ya kipigo cha mabao 2-0 kutoka kwa Tottenham Hotspur. Kikosi hicho cha Pep Guardiola kilianza msimu kwa ushindi mnono, wakati ilipoichapa Wolves mabao 4-0.

Haaland alisema msimu wao haupo vizuri na hivyo baada ya mapumziko ya mechi za kimataifa kupita, Man City sasa itashuka uwanjani Etihad kukabiliana na mahasimu wao, Man United katika mchezo wa Ligi Kuu England na hivyo straika huyo anataka ushindi upatikane.

“Tumepoteza mechi mbili mfululizo, hatupo kwenye kiwango bora, hii ni mbaya sana,” alisema Haaland.

“Tunapaswa kulitazama hili, kurudi kwenye njia zetu za ushindi. Haiwezekani kupoteza mechi nyingi. Ni wakati wa kuweka mambo sawa dhidi ya Man United. Sote tunahitaji kuwa kwenye viwango vyetu bora.”

Kocha Guardiola amekiri kikosi chake kuwa na mwanzo mbaya kwenye ligi na kuweka wasiwasi kama mafanikio waliyopata huko nyuma endepo kama yataweza kujirudia.