Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Haaland ndo hivyo tena Man City

Muktasari:

  • Straika Haaland alilazimika kutoka uwanjani kwenye mechi ya robo fainali ya Kombe la FA dhidi ya Bournemouth, Jumapili iliyopita.

MANCHESTER, ENGLAND: MANCHESTER City imefichua kwamba straika wao Erling Haaland huenda akakaa nje kwa siku kadhaa msimu huu baada ya kupata maumivu ya enka.

Straika Haaland alilazimika kutoka uwanjani kwenye mechi ya robo fainali ya Kombe la FA dhidi ya Bournemouth, Jumapili iliyopita.

Kocha wa Man City, Pep Guardiola amekuwa akiomba majeraha ya straika wake huyo yasiwe makubwa sana licha ya baadaye kuonekana akitembelea kwa msaada wa magongo.

Na kilichoonekana ni kama Haaland anaweza kuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu baada ya Man City kutoa taarifa yao iliyojaa wasiwasi wa mshambuliaji huyo.

Mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu England iliwaambia mashabiki wake kwamba Haaland amepata maumivu ya enka. Na kwamba alitarajia kukutana na mtaalamu kwa ajili ya kumfanyia vipimo zaidi kujua ukubwa wa tatizo.

Kwenye hilo ni kwamba Haaland anaweza kuwa nje ya uwanja kwa sehemu yote ya msimu huu, ikiwamo mechi ya nusu fainali ya Kombe la FA dhidi ya Nottingham Forest, lakini ikiaamini atarudi wakati wa Kombe la Dunia la Klabu.

Taarifa ya Man City ilisomeka hivi: “Manchester City inathibitisha kwamba Erling Haaland amepata maumivu ya enka ya mguu wa kushoto. Straika huyo wa Norway aliumia Jumapili kwenye mechi ya ushindi ya robo fainali ya Kombe la FA dhidi ya Bournemouth. Atafanyiwa vipimo zaidi Jumatatu asubuhi na mtaalamu kujua ukubwa wa tatizo.

“Atafanyiwa uchunguzi, matarajio ni kumwona Erling anakuwa fiti na kucheza tena sehemu ya msimu huu uliobaki ikiwamo Kombe la Dunia la Klabu. Tunamtakia Erling apone haraka na tutawaambia maendeleo yake.”

Mashabiki wa Man City wanaamini Haaland atarudi uwanjani haraka hasa katika kipindi hiki muhimu wanachohitaji huduma yake ili kumaliza msimu vizuri, baada ya kuondoka Bournemouth akiwa amevaa kiatu maalumu za maumivu.