Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Haaland amwaga mboga

Muktasari:

  • Man City ilitoka sare ya mabao 2-2 juzi dhidi ya AS Monaco licha ya kuongoza mechi kwa muda mrefu kabla ya kuruhusu bao la dakika za jioni lililofungwa na Eric Dier kwa njia ya penalti.

MANCHESTER, ENGLAND: STRAIKA wa Manchester City, Erling Haaland amesema kuwa timu yake sio nzuri vya kutosha baada ya kushindwa kupata ushindi katika mechi yao ya tano mfululizo kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Man City ilitoka sare ya mabao 2-2 juzi dhidi ya AS Monaco licha ya kuongoza mechi kwa muda mrefu kabla ya kuruhusu bao la dakika za jioni lililofungwa na Eric Dier kwa njia ya penalti.

Licha ya kupewa tuzo ya mchezaji bora wa mechi hiyo Haaland alionekana kuwa mwenye hasira sana na alipohojiwa alisema: “Sijikii vizuri kwa sababu hatukushinda mechi. Tulifanya mambo yasiyo ya lazima kipindi cha pili na sidhani kama tulicheza vizuri, hatukustahili kushinda na ndiyo maana tumepata matokeo haya.

Shida yetu kubwa hatukuwa tunajitoa kwa nguvu zaidi katika matukio, tunahitaji nguvu zaidi. Tulipaswa kucheza kwa kasi na nguvu kama tulivyofanya kipindi cha kwanza. Tulitawala zaidi, lakini kipindi cha pili wao walitumia nafasi zaidi na sidhani kama sisi tulicheza vizuri.

“Kila mechi ya Ligi ya Mabingwa ni ngumu, angalia mwaka jana tulitolewa. Kwa hiyo kila mchezo ni mgumu na si timu nyingi zimeshinda michezo yao miwili ya mwanzo.”

Haaland alifunga bao lake la kwanza katika mechi hiyo katika dakika ya 15 na kuongeza la pili katika dakika ya 44 ambalo liliwapa uongozi hadi dakika za mwisho ambapo Monaco ilisawazisha kwa penalti.

Man City itarejea katika EPLwikiendi hii ambapo itaumana na Brentford katika mechi ambayo inatarajiwa kuwa ya aina yake kutokana na matokeo ambayo timu hiyo imeyapata kwenye mechi iliyopita ambapo iliichapa Manchester United mabao 3-1.