Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Haaland aandika rekodi mpya England

Muktasari:

  • Straika huyo ameandikisha rekodi hiyo kwenye mechi dhidi ya Fulham baada ya kufunga bao katika dakika ya 17.

MANCHESTER, ENGLAND: STRAIKA wa Manchester City, Erling Haaland amekuwa mchezaji aliyefikisha mabao 100 kwa haraka zaidi ya mchezaji mwingine yeyote katika historia ya Ligi Kuu England.

Straika huyo ameandikisha rekodi hiyo kwenye mechi dhidi ya Fulham baada ya kufunga bao katika dakika ya 17.

Haaland, ambaye alitoka kapa kwenye mechi mbili zilizopita, sasa amekuwa mchezaji aliyefikisha mabao 100 kwa haraka zaidi kwenye Ligi Kuu England.

Imemchukua Haaland mechi 111 tu kufikisha idadi hiyo ya mabao 100, mechi 13 pungufu ya mchezaji anayemfuatia kwa kucheza mechi chache kufikisha mabao 100 kwenye Ligi Kuu England, Alan Shearer, ambaye alihitaji mechi 124.

Haaland sasa amefikisha mabao 15 kwenye ligi msimu huu na 20 katika michuano yote. Staa huyo wa kimataifa wa Norway, 25, amevunja rekodi kibao kwenye Ligi Kuu England tangu alipojiunga na Man City. Katika msimu wake wa kwanza aliandikisha rekodi mpya ya kufunga mabao mengi ndani ya msimu mmoja wa Ligi Kuu England, alipotikisa nyavu mara 36.

Haaland alikuwa mchezaji pia aliyefikisha mabao 50 haraka zaidi kwenye historia ya Ligi Kuu England, akifanya hivyo kwenye mechi 48, mechi 17 pungufu ya mchezaji anayemfuatia kwenye rekodi hiyo, Andy Cole, ambaye alihitaji mechi 65.

Kwa mwenendo wa kasi ya ufungaji ya Haaland, staa huyo yupo kwenye wakati mzuri wa kuvunja rekodi ya mabao kwenye Ligi Kuu England inayoshikiliwa na Shearer, ambaye amefunga 260.

Haaland alisema: “Nimekuwa na mwanzo mzuri na hili linanifanya nisikie vizuri. Nadhani hiki ni kipindi bora cha uwezo wangu. Sijawahi kusikia niko bora kuliko sasa.”


WACHEZAJI WALIOFIKISHA MABAO 100 KWA HARAKA KWENYE LIGI KUU ENGLAND

1.Erling Haaland - mechi 111

2.Alan Shearer - mechi 124

3.Harry Kane - mechi 141

4.Sergio Aguero - mechi 147

5.Thierry Henry - mechi 160