Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Gyokeres: Kile kikao cha moto kimesaidia

Muktasari:

  • Gyokeres, aliyetoa mchango wake katika mazungumzo hayo ya wazi, alikuwa mmoja wa nyota katika ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Tottenham Hotspur, Jumapili, akifunga mabao mawili na kudai yalikuwa matunda ya kikao chao cha pamoja.

LONDON, ENGLAND: STRAIKA, Viktor Gyokeres amedai kikosi cha Arsenal kilichokuwa kimevunjika moyo kilizidi kuwa karibu zaidi baada ya kikao cha moto cha ndani cha ndani walichowekana mastaa wa miamba hiyo ya Emitates.

Gyokeres, aliyetoa mchango wake katika mazungumzo hayo ya wazi, alikuwa mmoja wa nyota katika ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Tottenham Hotspur, Jumapili, akifunga mabao mawili na kudai yalikuwa matunda ya kikao chao cha pamoja.

Alipoulizwa kama kikao hicho kilikuwa cha moto, Gyokeres alisema: “Ndiyo, bila shaka. Nafikiri hicho ndicho tulichohitaji kufanya. Kama husemi ukweli, ni vigumu kuboresha mambo. Hilo ndilo jambo muhimu zaidi, kuwa mkweli, hasa katika timu hii. Kwa hiyo ndiyo, ilikuwa mazungumzo mazuri. Wengi wetu tulizungumza. Wakati mwingine ni muhimu kusema unavyohisi na kuyaweka wazi mbele ya kundi.

“Kila mtu anaweza kutambua jinsi wengine wanavyojisikia wakati huo na unapata uelewa mzuri zaidi wa hali. Unapozungumza waziwazi katika kundi, nafikiri mnazidi kuwa karibu zaidi na hilo ni jambo muhimu kufanya mara kwa mara.”

Gyokeres sasa amefikisha mabao 10 Ligi Kuu England baada ya kufunga mara mbili dhidi ya Spurs na anaamini huo ulikuwa mchezo wake bora tangu ajiunge na Arsenal akitokea Sporting CP kwa ada ya Pauni 54.8 milioni.

Alisema: “Nikiwa nahusika kama nilivyokuwa kwenye mechi ile na kupata mipira karibu na eneo la hatari, inakuwa rahisi kuonyesha ubora wangu na kufunga mabao. Mimi napenda kufunga, haijalishi tunacheza na nani, lakini katika mechi ya aina hii ni jambo la kufurahisha zaidi kufunga.

“Jambo muhimu ni kuendelea kuonyesha kiwango hiki katika mechi inayofuata na ile itakayofuata. Bado kuna mechi nyingi. Tukicheza hivi, mambo yatakuwa mazuri, bila shaka.”

Gyokeres pia alifichua alifurahia kucheza pamoja na Eberechi Eze, ambaye pia alifunga mabao mawili na kufikisha jumla ya mabao matano dhidi ya Spurs msimu huu, aliposema: “Unapokuwa na namba 10 mwenye ubora kama wake, inakuwa rahisi sana. Pia wachezaji kama Martin Odegaard na Kai Havertz. Inasaidia sana.”

Aidha, kiungo Declan Rice alifichua kuwa wachezaji waliokuwa na wasiwasi waliitisha kikao hicho Ijumaa ili kujadili sare ya kusikitisha ya mabao 2-2 dhidi ya Wolves, Jumatano, matokeo yaliyomaanisha walikuwa wameshinda mara mbili tu katika mechi saba za ligi.