Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Gyokeres bado shida iko hapa

Muktasari:

  • Kocha Mikel Arteta alikuwa akijiandaa kumpokea straika huyo baada ya klabu mbili kufikia makubaliano ya ada ya Pauni 63.5 milioni.

LISBON, URENO: DILI la Arsenal la kumnasa straika Viktor Gyokeres lipo kwenye hatari ya kuvunjika, imeripotiwa.

Kocha Mikel Arteta alikuwa akijiandaa kumpokea straika huyo baada ya klabu mbili kufikia makubaliano ya ada ya Pauni 63.5 milioni.

Lakini, mambo bado yamekwama kwenye ishu ya bonasi wanayotaka Sporting ilipwe.

Kinachoelezwa ni kwamba Sporting inaripotiwa kuhitaji Pauni 8.7 milioni tofauti na lile dili la awali walilokubaliana.

Arsenal inadaiwa kutokubaliana na hilo la bonasi, ambapo Sporting inataka kiwepo kabisa kipengele kwenye mkataba wake. Hilo ndilo linaloweka dili hilo la Gyokeres kuwa kwenye hatari kubwa ya kuvunjika katika hatua za mwisho kabisa.

Rais wa Sporting, Frederico Varandas anaripotiwa kushikilia msimamo huo. Lakini, moyo wa mchezaji Gyokeres, 27, tayari umeshajielekeza kwenda kucheza Emirates, ambako inaaminika atakwenda kusaini mkataba wa miaka mitano.

Wikiendi iliyopita, Varandas alisema Gyokeres anaweza kukabiliana na adhabu endapo kama ataendelea kukosekana kwenye kambi ya mazoezi ya timu hiyo ambayo ilipaswa kuwapo huko Algarve, Jumamosi.

Gyokeres, ambaye alifunga mabao 54 katika mechi 52 alizocheza msimu uliopita na kubeba mataji mawili ikiwamo la ligi, bado hajaeleza hadharani kwanini hataki kwenda kuungana na wenzake kwenye mazoezi ya pre-season.