Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Gyokeres awakataa mabosi Sporting Lisbon

GYOKERES Pict

Muktasari:

  • Mshambuliaji huyo wa kimataiwa wa Sweden anawaniwa na timu kubwa za Ligi Kuu England  hususani Manchester United na Arsenal  zinazomhitaji katika dirisha hili la usajili la majira ya kiangazi.

LISBON, URENO: STRAIKA wa Sporting Lisbon, Viktor Gyokeres amekataa ombi la kufanya mazungumzo na viongozi wa timu yake huku sakata lake la uhamisho likizidi kuchukua suta mpya.

Mshambuliaji huyo wa kimataiwa wa Sweden anawaniwa na timu kubwa za Ligi Kuu England  hususani Manchester United na Arsenal  zinazomhitaji katika dirisha hili la usajili la majira ya kiangazi.

Kwa muda, Arsenal ilionekana kuwa na nafasi nzuri ya kumnasa, hasa baada ya Gyokeres kuonyesha nia ya kuhamia Kaskazini mwa London.

Hata hivyo, uhamisho huo unaonekana kuwa mbali kukamilika  kwa sasa baada ya Sporting kuibuka na kusisitiza hawatomuuza kwa bei ya chini.

Hali hiyo imemkasirisha sana Gyokeres, ambaye anaamini timu hiyo ya Ureno imekiuka ahadi yao ya kumuacha aondoke.

Kutokana na hilo, inaelezwa staa huyo ametoa tishio la kugoma kuungana na timu na kucheza msimu ujao ili kulazimisha kuondoka.

Sporting walijaribu kupunguza mvutano huo kwa kutaka kufanya mazungumzo naye, lakini ombi hilo  alilikataa.

Kwa mujibu wa  tovuti ya Record, Sporting walitaka kuzungumza na Gyokeres ili  kuelewana, lakini wawakilishi wake walikataa pendekezo hilo.

Wakati hayo yakiendelea, nyota huyo wa zamani wa Coventry City bado yuko likizo huko Saint Tropez, Ufaransa na hatarajiwi kurejea kambini hivi karibuni.

Gyokeres mwenyewe katika ukurasa wake wa Instagram wiki iliyopita alifunguka kidogo kuhusu  yanayoendelea akisema: “Kuna maneno mengi yanayozungumzwa kwa sasa, mengi kati yake si ya kweli. Nitasema wakati utakapofika.”

Kwa upande mwingine, Rais wa Sporting, Frederico Varandas, amezungumza kuhusu sakata hilo na kusisitiza hawatalazimishwa kumuuza Gyokeres.

Alisema: “Jambo moja unalopaswa kujua ni hunitishi. Vitisho, hila na matusi havifanyi kazi kwangu.”

“Ninathibitisha Viktor Gyokeres hatouzwa kwa Euro 70 milioni kwa sababu sijawahi kumuahidi hivyo. Hii michezo ya wakala wake inazidi kuharibu hali. Mpaka sasa, Sporting haijapokea ofa yoyote kwa Viktor.”