Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Gyokeres aaanza kuhamisha vitu

GYOKERES Pict

Muktasari:

  • Staa huyo wa Sporting anakaribia kukamisha uhamisho wake wa pesa nyingi kutua huko London hasa baada ya kugomea kurudi kwenye mazoezi ya timu ya Sporting.

LISBON, URENO: ARSENAL ipo kwenye hatua za mwisho za kukamilisha dili la Pauni 69 milioni la kumsajili straika Viktor Gyokeres baada ya gari la kuhamisha vyombo kuonekana mbele ya nyumba ya staa huyo huko Lisbon, Ureno.

Staa huyo wa Sporting anakaribia kukamisha uhamisho wake wa pesa nyingi kutua huko London hasa baada ya kugomea kurudi kwenye mazoezi ya timu ya Sporting.

Lakini, kwa sasa Arsenal sasa ipo nyuma kwa Pauni 4 milioni tu kukamilisha dili hilo.

Na straika Gyokeres anaonekana sasa kujiandaa kutua Emirates baada ya kuanza kuhamisha vitu vyake huko Lisbon.

Picha zimesambaa mtandaoni zikionyesha gari la kuhamisha vitu likiwa mbele ya nyumba ya kifahari ya Gyokeres huko Lisbon. Kilichokuwa kikiaminika staa huyo alibaki Sweden baada ya kuwaambia mabosi wa Sporting harudi tena Ureno. Na kwenye mitandao pia ilionekana staa huyo akipanda kwenye ndege binafsi kutoka Stockholm kwenda London kwa ajili ya kukamilisha mipango yake. Hata hivyo, taarifa nyingine zinadai kwamba hakukuwa na uhakika kama ndege hiyo ilimbeba Gyokeres.

Lakini, jambo hili liliwafurahisha zaidi mashabiki wa Arsenal na kuvamia kwenye mitandao ya kijamii, ambapo mmoja alisema: “Karibu kwenye klabu kubwa duniani.”€

Mwingine aliongeza: “Mungu awabariki mashabiki wa Arsenal wa mtandaoni.”€

Arsenal bado ipo kwenye msako wa kumfukuzia winga wa Crystal Palace, Eberechi Eze.