Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Guardiola kuamua hatma yake Jumapili Carabao Cup

Muktasari:

  • Kocha huyo, 55, kwa sasa yuko katika miezi 18 ya mwisho ya mkataba wake wa miaka miwili aliouongeza mwaka 2024.

MANCHESTER, ENGLAND: KOCHA wa Manchester City, Pep Guardiola atafanya uamuzi kuhusu mustakabali wake baada ya fainali ya Kombe la Carabao dhidi ya Arsenal, Jumapili ya wiki hii.

Kocha huyo, 55, kwa sasa yuko katika miezi 18 ya mwisho ya mkataba wake wa miaka miwili aliouongeza mwaka 2024.

Kwa mujibu wa Daily Mail, Guardiola atafanya uamuzi siku chache baada ya mechi hiyo dhidi ya washika mitutu itakayopigwa Uwanja wa Wembley.

Ikiwa Guardiola ataondoka kuna uwezkano mkubwa aliyekuwa kocha wa Chelsea, Enzo Maresca, akamrithi.

Man City ilitolewa kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya na wapinzani wa zamani wa Guardiola, Real Madrid, baada ya kichapo cha  jumla cha mabao 5-1.

Vinicius Jr alifunga mabao mawili katika mchezo wa mkondo wa pili na mambo yalionekana kuharibika zaidi kwa Man City baada ya Bernardo Silva kuonyeshwa kadi nyekundu ya moja kwa moja kwa kushika mpira kwa mkono.

Ripoti zinadai mkurugenzi wa michezo wa Man City, Hugo Viana, tayari ameanza kutafuta mbadala wa Guardiola ambaye atachukua mikoba yake ikiwa ataondoka.

Kwa sasa Man City ipo nafasi ya pili katika msimamo wa ligi ikiwa na tofauti ya alama tisa dhidi ya vinara Arsenal.

Akizungumza baada ya mechi yao ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Madrid, wiki hii, Guardiola alisema licha ya kutolewa bado walijitahidi sana.

"Ni vigumu kushinda mechi unapokuwa nyuma kwa mabao 4-0 na unacheza watu 10 dhidi ya 11. Tuna timu ya kipekee, Mustakabali wa kikosi ni mzuri, tumepata kitu cha kujifunza kidogo."