Giroud apiga nne, Neymar aichakaza Man United

Thursday December 03 2020
giround pic

SEVILLE, HISPANIA. Olivier Giroud alikuwa na usingizi mtamu baada ya jana Jumanne usiku kuiongoza Chelsea kuichapa Sevilla mabao 4-0 huku yeye akifunga mabao yote wakati Manchester United imekutana na kipigo cha mabao 3-1 kutoka wa PSG.

Mabao hayo manne ya Giroud yameifanya Chelsea kuendeleea kujikita kileleni mwa msimamo wa kundi E baada ya kufikisha pointi 13.

Hata hivyo Kilichotokea huko Old Trafford unaweza kusema kuwa ilikuwa ni kizaazaa  baada ya Machester United  kujikuta ikikumbana na kipigo cha mabao 3-1 na aliyekuwa mwiba kwao alikuwa ni staa Neymar ambaye alitupia mabao mawili kwenye mchezo huo.

Katika mchezo huo, Manchester United ilijikuta ikimaliza pungufu baada ya kiungo wao mkabaji, Fred kuonyeshwa kadi nyekundu.

Kwa matokeo hayo, Manchester United bado hawana uhakika wa kutinga hatua ya mtoano licha ya kuendelea kuongoza msimamo wa kundi H ikiwa na pointi tisa sawa na timu mbili zilizo kwenye nafasi ya pili na tatu ambazo ni PSG na RB Leipzig.

Michezo ya raundi ya mwisho ya hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya ndiyo itakayoamua hatma ya vijana hao wa Ole Gunnar Solskjaer ambapo wenyewe wataikabili  RB Leipzig.

Advertisement

MATOKEO KWA UJUMLA

Basaksehir 3- 4 RB Leipzig
Krasnodar 1-0 Rennes
Club Brugge KV 3- 0 Zenit
Dortmund 1- 1 Lazio
Ferencvaros 0- 3 Barcelona
Juventus 3- 0 Dyn. Kyiv
Manchester Utd 1- 3 Paris SG
Sevilla 0- 4 Chelsea

Advertisement