Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Gerrard afufua bifu na El-Hadji Diouf

GERRARD Pict

Muktasari:

  • Gerrard na Diouf walicheza pamoja katika klabu ya Liverpool kati ya mwaka 2002 hadi 2004, kabla Msenegali huyo hajaondoka kujiunga na Bolton Wanderers na ni wazi kuwa wawili hao hawakuwa na uhusiano mzuri.

LIVERPOOL, ENGLAND: NAHODHA wa zamani wa Liverpool, Steven Gerrard, amemrushia maneno ya kejeli aliyekuwa mchezaji mwenzake El-Hadji Diouf, akifufua tena bifu lao la muda mrefu lililoanza zaidi ya miaka 20 iliyopita.

Gerrard na Diouf walicheza pamoja katika klabu ya Liverpool kati ya mwaka 2002 hadi 2004, kabla Msenegali huyo hajaondoka kujiunga na Bolton Wanderers na ni wazi kuwa wawili hao hawakuwa na uhusiano mzuri.

Siku ambayo Gerrard alitangaza kustaafu soka, Diouf alizungumza tena kwenye televisheni ya Ufaransa, na kufufua upya ugomvi huo wa muda mrefu.

Diouf amewahi kumtuhumu Gerrard kuwa ni mwenye wivu, mbinafsi, na hata mbaguzi wa rangi, madai ambayo Gerrard ameyakanusha vikali. Gerrard naye amekuwa akifichua wazi kuwa hakupendezwa na tabia wala mtazamo wa Diouf kuhusu soka na maisha kwa ujumla.

Gerrard alifichua kutompenda Diouf kwa mara ya kwanza mwaka 2007 kupitia wasifu wake wa kwanza. Aliandika: “Sikuwa shabiki wa Diouf. Nilijua ni wachezaji gani waliojitoa kwa Liverpool na waliokuwa na njaa ya mafanikio, lakini Diouf alikuwa anajali zaidi maslahi yake binafsi.”

GERRA 01

Mwaka 2012, Diouf alipokuwa akiichezea Leeds United, alijibu tuhuma hizo kwa kudai kuwa “hakuna mtu Liverpool aliyempenda Gerrard”, licha ya Gerrard kuwa nahodha aliyewaongoza kushinda Ligi ya Mabingwa Ulaya mwaka 2005.

Katika mahojiano mapya na Rio Ferdinand, Gerrard amefufua tena hoja hiyo alipoulizwa kuhusu usajili wa wachezaji wa Liverpool wakati wake.

Gerrard amesema: “Tulifanya makosa makubwa ya usajili nyakati fulani. Nitakupa mfano mmoja tulikuwa na nafasi ya kumsaini Nicolas Anelka au El-Hadji Diouf. Tukamnunua Diouf kwa sababu ya mechi chache nzuri alizocheza kwenye fainali za Kombe la Dunia, badala ya Anelka ambaye alikuwa na kiwango cha juu kwa miaka kadhaa. Hilo lilikuwa kosa kubwa.”

Ameongeza: “Sijui nani alifanya uamuzi wa mwisho, lakini huo ulikuwa mfano wa wazi kabisa wa makosa ya usajili. Anelka alikuwa mchezaji wa kiwango cha juu sana kuliko Diouf.”

Anelka alichezea Liverpool kwa mkopo kati ya Desemba 2001 na Mei 2002, lakini klabu haikumwajiri kwa kudumu ndipo Diouf aliponunuliwa majira ya kiangazi ya 2002.

GERRA 02

Rio Ferdinand amesema: “Anelka ni mmoja wa washambuliaji wagumu zaidi niliowahi kukutana nao, yuko kwenye tatu bora kwa ugumu.”

Gerrard akajibu: “Anelka alikuwa mtulivu, mwenye kujiamini, na alikuwa tayari kutusaidia kushinda zaidi. Lakini klabu ikachagua tofauti, na hilo lilikuwa kosa kubwa.”


Historia ya Bifu Lao

2002–2004: Gerrard na Diouf walicheza pamoja Liverpool, lakini haikuwahi kuwa na urafiki kati yao. Gerrard alimkosoa Diouf kwa ukosefu wa kujituma, akisema alikuwa hajali klabu.


2007: Katika wasifu wake wa kwanza, Gerrard amesema wazi kuwa Diouf alikuwa mchezaji ambaye hakujali timu na alikuwa na mtazamo mbaya.


2012: Diouf alijibu akiwa Leeds, akidai Gerrard alikuwa na wivu kwa mafanikio yake akiwa na timu ya taifa ya Senegal, na kwamba wachezaji wengi Liverpool hawakumpenda Gerrard.

GERRA 03

2015: Katika kitabu chake cha pili My Story, Gerrard alimkosoa Diouf tena, akisema alikuwa mfano wa jinsi usajili unaweza kuharibika. Alimkumbusha tukio la mwaka 2003 alipomtemea mate shabiki wa Celtic, akisema lilionesha tabia yake ya kudharau wengine.


2015: Baada ya kitabu hicho, Diouf alidai Gerrard “hajawahi kuwapenda watu weusi”, madai ambayo Gerrard aliyakana kupitia wakili wake na kuyaita “ya kipuuzi na ya kibaguzi”.


2016: Diouf aliendelea kumkejeli Gerrard, akisema mafanikio yake na timu ya Senegal yalikuwa makubwa kuliko yote aliyowahi kuyapata Gerrard na England. Pia alimcheka Gerrard kwa “utelezi” wake dhidi ya Chelsea mwaka 2014 uliogharimu Liverpool ubingwa.


2016 (Novemba): Baada ya Gerrard kustaafu, Diouf alisema kwenye televisheni ya Ufaransa kuwa “Gerrard alikuwa si kitu chochote” na kwamba hakuwahi kufanya kitu cha maana katika mashindano makubwa.