Gavi amerudi mzigoni
Muktasari:
- Kiungo huyo wa kimataifa wa Hispania mwenye umri wa miaka 21 alipata jeraha baya la goti mwezi Agosti lililomlazimu kukaa nje ya uwanja kwa muda mrefu.
BARCELONA, HISPANIA: KOCHA wa FC Barcelona, Hansi Flick amesema kiungo wake Gavi yuko tayari kurejea uwanjani baada ya kukaa nje kwa muda mrefu kutokana na majeraha.
Kiungo huyo wa kimataifa wa Hispania mwenye umri wa miaka 21 alipata jeraha baya la goti mwezi Agosti lililomlazimu kukaa nje ya uwanja kwa muda mrefu.
Flick alisema anafurahia kurejea kwa kiungo huyo na anaweza kupewa dakika chache za kucheza kulingana na hali yake.
Kocha huyo alieleza katika mazoezi Gavi ameonekana kuwa na nguvu na ari kubwa ya kucheza, jambo linaloonyesha kuwa ameanza kurejea katika kiwango chake.
Hata hivyo, Flick alisisitiza ni muhimu kumuangalia kwa karibu ili kuhakikisha hapati tatizo jingine la kiafya.
Gavi pia alikosa sehemu kubwa ya msimu wa 2023/2024 kutokana na jeraha jingine la goti, lakini anatajwa kuwa mmoja wa viungo wa nguvu ambao Barcelona wamekuwa wakimkosa katika safu yao ya kiungo msimu huu.
Barcelona inatarajiwa kucheza dhidi ya Newcastle United katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa katikati ya wiki.