Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Garnacho awatibua mashabiki Man United

GERNACHO Pict

Muktasari:

  • Garnacho, 20, ameambiwa na kocha wa Man United, Ruben Amorim kutafuta timu mpya ya kwenda kujiunga nayo baada ya kushindwa kuonyesha kiwango bora msimu uliopita.

MANCHESTER, ENGLAND: MASHABIKI wa Manchester United kwa hasira wametuma meseji za kumfukuza staa wao Alejandro Garnacho baada ya kuonekana akiwa amevaa jezi ya Aston Villa yenye jina la Marcus Rashford.

Garnacho, 20, ameambiwa na kocha wa Man United, Ruben Amorim kutafuta timu mpya ya kwenda kujiunga nayo baada ya kushindwa kuonyesha kiwango bora msimu uliopita.

Staa huyo wa Kiargentina alifunga mabao sita kwenye Ligi Kuu England. Na sasa mchezaji huyo ameanza kutafuta timu mpya, huku Napoli na Chelsea zikionyesha dhamira ya dhati kuhitaji huduma yake.

Kwa sasa, Garnacho yupo likizo na ameonekana Rome, Italia na Tokyo, Japan. Na hivi karibuni, alionekana kwenye visiwa vya starehe huko Hispania, Ibiza.

Na Garnacho alionekana kama vile ameshafanya uamuzi wa kuhusu hatima yake kwenye kikosi cha Man United baada ya kupiga picha akiwa na jezi ya timu nyingine na wala hakuonekana kuwa na shida. Garnacho alivaa jezi ya Aston Villa, yenye jina la Rashford, staa mwingine wa Man United, ambaye nusu ya pili ya msimu uliopita aliichezea timu hiyo ya Villa Park kwa mkopo. Garnacho na Rashford wote hawaonekani kuwa na maisha kwenye kikosi cha Man United chini ya kocha Amorim, sambamba na winga mwingine, Antony.

Lakini, kitendo cha Garnacho kimeibua mashabiki wa timu hiyo na mmoja alisema: “Toka klabuni kwetu.”

Mwingine alisema: “Huu ni ujinga.”

Kuna shabiki mwingine alisema: “Hii ndio maana tunataka kubadili utamaduni.” Huku mwingine akisema: “Anaomba kuondoka.” Kuna shabiki mwingine alisema: “Achaneni naye.”