Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Fernandes afunguka ishu ya kuondoka Man United

Muktasari:

  • Kiungo Fernandes alihusishwa na mpango wa kuhamia Al-Hilal mapema kwenye dirisha hili la uhamisho wa majira ya kiangazi, lakini aligomea ofa hiyo.

MANCHESTER, ENGLAND: NAHODHA wa Manchester United, Bruno Fernandes ameripotiwa kufungua milango ya kuachana na timu hiyo kwenye dirisha la majira ya kiangazi mwakani baada ya kugomea ofa tamu kabisa kutoka Saudi Arabia.

Kiungo Fernandes alihusishwa na mpango wa kuhamia Al-Hilal mapema kwenye dirisha hili la uhamisho wa majira ya kiangazi, lakini aligomea ofa hiyo.

Al-Hilal iliweka mezani ofa ya Pauni 100 milioni na ilikuwa tayari kumpa Fernandes mshahara wa Pauni 700,000 kwa wiki, kitu ambacho kingemfanya avune Pauni 200 milioni kwenye dili la miaka mitatu.

Hata hivyo, kwa siku za karibuni alihusishwa pia na klabu nyingine ya Saudi Pro League, ambapo Al-Ittihad iliripotiwa kuzungumza na mawakala wa Fernandes.

Lakini, ripoti zinafichua kwamba Fernandes bado anataka kuendelea kubaki Man United walau kwa mwaka mmoja ili asitibue mipango yake ya kwenda kwenye fainali za Kombe la Dunia 2026.

Na kinachoelezwa ni kwamba supastaa huyo wa Ureno ataanza kufikiria kuondoka baada ya fainali hizo za Kombe la Dunia 2026.

Ripoti nyingin zinadai Fernandes amefunga milango ya kwenda Saudi Arabia, Amerika au kwenye ligi nyingine kubwa za Ulaya itakapofika dirisha la mwakani.

Alipozungumzia kugomea ofa ya Al-Hilal, Fernandes aliambia Sky Sports mapema mwezi huu: "Bado sijakamilisha ndoto zangu mahali hapa. Nadhani bado kuna kitu naweza kukifanya kwenye klabu. Nadhani bado nipo kwenye nafasi ya kufanya jambo na nitaendelea kubaki hadi klabu itakaponiambia Bruno sasa ni muda wa kuondoka."