Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ferguson aonya kitu Man United

Muktasari:

  • Man United imeshindwa kufurukuta kwenye Ligi Kuu England tangu kocha huyo Mskochi alipojiuzulu 2013 na taji lao la mwisho kubeba kwenye ligi lilikuwa msimu wa 2012/13.

MANCHESTER, ENGLAND: SIR Alex Ferguson amesema inaweza kuwachukua Manchester United miaka mingine 10 kabla ya kunyakua tena taji la Ligi Kuu England. Lakini, gwiji huyo wa Man United amemwangushia mzigo wote kocha Ruben Amorim.

Man United imeshindwa kufurukuta kwenye Ligi Kuu England tangu kocha huyo Mskochi alipojiuzulu 2013 na taji lao la mwisho kubeba kwenye ligi lilikuwa msimu wa 2012/13.

Miamba hiyo ya Old Trafford tangu wakati huo imebadilisha makocha wakuu sita na kufanikiwa kushinda mataji matano, lakini hakuna hata moja la Ligi Kuu England.

Si David Moyes, Louis van Gaal, Jose Mourinho, Ole Gunnar Solskjaer wala Erik ten Hag walioweza kufikia mafanikio ya Ferguson aliyopata wakati anakinoa kikosi hicho cha Old Trafford.

Man United ilimaliza kwenye nafasi ya 15 katika msimamo msimu uliopita, ikiwa ni nafasi ya chini kuwahi kushika katika zama za Ligi Kuu England na ilikosa fursa ya kucheza kwenye michuano ya Ulaya baada ya kupoteza kwenye mechi ya fainali ya Europa League dhidi ya Tottenham Hotspur.

Ferguson, ambaye alibeba mataji makubwa 38 akiwa na Man United, alisema itachukua muda mrefu kabla ya timu hiyo haijawa bingwa wa England tena. Lakini, alimsifu Amorim, aliposema: "Amorim ana sera zake. Sio mtu mrahisi. Nakumbuka mimi katika kipindi changu, nilianza wakati Liverpool ikiwa moto. Ilikuwa klabu bora na ilishinda mataji manne ya Ulaya wakati huo, lakini iliwachukua miaka 31 kushinda ubingwa wa ligi tena.

"Kwa sasa yupo kwenye hali hiyo. Inaweza kuchukua miaka 10, inaweza kuwa miaka 11 kwa sababu huu ni kama mzunguko. Hili linapaswa kufanyiwa kazi vyema na tunapaswa kuzingatia usajili wetu unakwenda kuwa bora kuliko ilivyo sasa."

Licha ya mambo kuwa hovyo kwa zaidi ya muongo sasa, Ferguson anadhani usajili uliofanyika dirisha lililopita la majira ya kiangazi ulikuwa mzuri kwa Man United. Senne Lammens, Bryan Mbeumo na Matheus Cunha wote wamekuwa na mchango mzuri kwenye kikosi hicho cha kocha Amorim.

"Nadhani usajili wa kipa Lammens umeleta tofauti," alisema gwiji huyo na kuongeza. "Ni kijana wa miaka 23, mwepesi na ana mwili mkubwa, yupo vizuri miguu na mikononi, nadhani hilo limesaidia. Nadhani tunahitaji mchezaji wa aina yake. Man United siku zote imekuwa na wachezaji wanaohamasisha. Nadhani hilo limesaidia sana. Wachezaji wengine wawili, Mbeumo na Cunha, wanaonekana kama kuna kitu watakifanya katika kuhakikisha tunarejea kwenye ubora wetu."

Man United itashuka uwanjani Villa Park usiku wa Jumapili kukipiga na Aston Villa katika kivumbi cha Ligi Kuu England.