Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Eze, Guehi kutuliza mzuka

EZE Pict

Muktasari:

  • Liverpool, Newcastle na Tottenham zimekuwa zikimfukuzia beki wa England, Guehi, wakati Arsenal bado inafukuzia saini ya Eze.

LONDON, ENGLAND: BEKI wa kati, Marc Guehi na kiungo mshambuliaji Eberechi Eze huenda wote wakabaki Crystal Palace msimu huu baada ya mastaa hao kuwindwa na timu kibao.

Liverpool, Newcastle na Tottenham zimekuwa zikimfukuzia beki wa England, Guehi, wakati Arsenal bado inafukuzia saini ya Eze.

Licha ya kwamba bado karibu mwezi mzima wa dirisha la usajili, lakini kinachoonekana kwa sasa mastaa hao wanaweza kubaki Selhurst Park.

Palace haijapokea ofa yoyote kuhusu wachezaji hao na hawana haraka ya kuwauza. Hiyo ni habari njema kwa mashabiki wa klabu hiyo ambao wanaamini uwepo wa wachezaji hao kwenye timu yao itakuwa kwenye uimara mkubwa.

Liverpool imekuwa ikipewa nafasi ya kumnasa beki wa kati Guehi na imeshazungumza na mawakala wa mchezaji huyo. Beki huyo mkataba wake umebaki mwaka mmoja tu huko Selhurst Park, lakini halazimishi kuuzwa.

Liverpool inamthaminisha Guehi kuwa na thamani ya Pauni 40 milioni, ikiwa ni pungufu kwa Pauni 10 milioni kwenye bei ambayo Palace wanataka.

Spurs nayo bado inamtaka baada ya ofa yao ya Pauni 70 milioni kwenye dirisha la Januari ilikataliwa na Palace. Newcastle nayo inamtaka, lakini ofa yao ipo nyuma kwa Pauni 10 milioni kwa kiwango ambacho Palace inakitaka.

Guehi amekuwa akihusishwa pia na klabu za Barcelona na Real Madrid zinahitaji huduma yake.

Kiungo mshambuliaji Eze amekuwa kwenye mipango ya Arsenal wakihitaji saini yake akakipige huko Emirates. Arsenal inajiandaa kulipa Pauni 68 milioni kama kiwango cha pesa kilichowekwa kwenye mkataba wake ili kuvunjwa.