Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Europa League, Conference League zapamba moto leo robo fainali

Muktasari:

  • Usiku wa leo, Alhamisi, Aston Villa inaingia kwenye mchezo wa marudiano wa robo fainali ya Europa ikiwa na faida kubwa baada ya ushindi wa mabao 3-1 walioupata Italia dhidi ya Bologna FC 1909.

LONDON, ENGLAND: UKISIKIA funga kazi basi ndio hii. Baada ya usiku wa jana, Jumatano, kumalizika kwa kishindo kwa michezo ya robo fainali za Ligi ya Mabingwa Ulaya, leo ndio hesabu za michuano midogo ya Europa na Conference League zinafungwa katika robo fainali. 

Usiku wa leo, Alhamisi, Aston Villa inaingia kwenye mchezo wa marudiano wa robo fainali ya Europa ikiwa na faida kubwa baada ya ushindi wa mabao 3-1 walioupata Italia dhidi ya Bologna FC 1909. Matokeo hayo yamewapa Villa nafasi nzuri ya kufuzu ya kutinga nusu fainali huku wakihitaji kulinda uongozi wa mabao hayo katika mchezo wa nyumbani.

Chini ya kocha Unai Emery, Aston Villa wamekuwa katika kiwango bora sana msimu huu wa Europa, wakishinda michezo 10 kati ya 11 ya mwanzo, jambo linaloonyesha ubora wa kikosi chao. Rekodi yao ya nyumbani pia inatisha, kwani wameshinda mechi 15 kati ya 17 za mwisho za mashindano ya Ulaya na sasa wameshinda mechi nane mfululizo bila kupoteza uwanja wao wa nyumbani.

Kwa upande wa Bologna, kazi ni kubwa mno kwani wanahitaji kurudisha tofauti ya mabao mawili ugenini, jambo ambalo kihistoria ni gumu sana katika mashindano haya. Hata hivyo, timu hiyo imeonyesha uimara ugenini kwa kushinda mechi zao zote tano za Europa zilizo fuatia tangu walipopoteza dhidi ya Villa mapema msimu huu katika hatua zilizopita na pia wamekuwa wakifunga mabao katika mechi 19 mfululizo za ugenini.

Villa pia wana rekodi nzuri dhidi ya timu za Italia wakiwa nyumbani, huku Bologna wakiwa na kumbukumbu mbaya dhidi ya timu za England barani Ulaya.

Wachezaji kama Ollie Watkins na John McGinn wanakaribia kuandika historia ya klabu hiyo ya Enhgland kwa kufikisha mabao 10 ya Ulaya kila mmoja, wakati Bologna wakimtegemea Federico Bernardeschi ambaye ndiye mfungaji wao bora kwenye mashindano haya.

Mechi nyingine kubwa na nzuri ya kutazama ni kati ya Nottingham Forest dhidi ya Porto ambapo katika mechi ya kwanza walitoka sare ya bao 1-1 Ureno, hivyo mechi hii ya marudiano huko England ni kama iaanza upya vile.

Forest wanaingia kwenye mchezo huu wakiwa na changamoto kubwa, sio kwenye mashindano ya Ulaya bali pia kwenye ligi ya England. Timu hiyo bado inahusishwa na vita ya kuepuka kushuka daraja na licha ya sare ya bao 1-1 dhidi ya Aston Villa mwishoni mwa wiki, bado wako karibu na ukanda wa hatari. Hata hivyo, rekodi yao nyumbani kwenye mashindano ya Ulaya si nzuri, kwani wamepoteza mechi tatu katika uwanja wao wa City Ground msimu huu na kupoteza tena kunaweza kuwaweka kwenye historia mbaya ya kuwa timu ya kwanza ya England kupoteza mechi nne za nyumbani katika msimu mmoja wa mashindano makubwa ya Ulaya.

Kwa upande wa Porto, mambo yako tofauti kabisa. Timu hiyo inaongoza ligi ya Ureno ‘Liga Portugal’ wakiwa na pointi tano mbele baada ya ushindi wa 3-1 dhidi ya Estoril Praia na sasa wanaingia kwenye mchezo huu wakiwa kwenye mfululizo wa mechi nane bila kupoteza (wakiwa na ushindi wa mechi tano na sare tatu).

Porto pia wamekuwa bora wakiwa ugenini, wakishinda mechi zao tatu za mwisho, ikiwa ni pamoja na ushindi muhimu dhidi ya Stuttgart kwenye hatua iliyopita ya mashindano haya. Hata hivyo, historia yao katika mechi za marudiano za Ulaya sio nzuri sana, kwani wameshinda mechi nne tu kati ya 22 za marudiano za mashindano makubwa ya Ulaya.

Mechi nyingine ambazo zinatarajiwa kupigwa leo ni Celta Vigo itakuwa nyumbani ikiwa na kibarua cha kuchomoa mabao 3-0 waliyofungwa Ujerumani dhidi ya Freiburg huku Real Betis na Braga wao mechi yao ikianza upya kufuatia kutoa sare ya bao 1-1 kwenye mechi ya kwanza.