Eti Ancelotti amezingua kinoma

LONDON, ENGLAND. MCHAMBUZI wa soka wa kituo cha televisheni BT, Rio alishangwazwa na kitendo cha kocha Carlo Ancelotti kutompanga Antonio Rudiger, badala yake akamchezesha Eder Militao katika mechi ya marudiano ya nusu fainali ya Ligi Mabingwa Ulaya dhidi ya Manchester City.

Rudiger alicheza kwa kiwango bora katika mechi ya kwanza uwanja wa Santiago Bernabeu, Militao alipoondolewa kikosini kutokana na kutumikia adhabu, Madrid ikalazimishwa sare ya bao 1-1 dhid ya Man City.

Katika mchezo huo wa kwanza Rudiger alimzuia straika Erling Haaland asilete madhara eneo la hatari dakika zote za mchezo lakini Rio akashangazwa Rudiger alivoachwa nje kikosi cha kwanza katika mechi hiyo ya marudiano.

Alipoulizwa kuhusu mabadiliko hayo aliofanya Ancelotti, Rio aliiambia BT Sport: "Hata sielewi kwanini Rudiger aliachwa benchi, wakati mwingine unafikiria hivi tulishuhudia kumuona beki ambaye angemzuia Haaland? inashangaza kwakweli, kama Rudiger ana namba nzuri basi angeendelea naye tu, Ancelotti alikuja na kitu ambacho anakiamini, Rudiger alikuwa na kiwango bora tangu msimu uliopita aliwasaida sana, unawezaje kumuacha benchi mtu ambaye ni mhimili wa timu?, Huwezi kataa Militao ni chuguo namba moja kikosini, je alikuwa na mchango zaidi msimu wote huu? kama ningekuwa mimi ningefikiria zaidi, kwa kilichotokea amezingua Ancelotti," alisema Rio

Kipigo cha mabao 4-0 walichopata hayakuwa ambayo Ancelotti ametaka katika kusherehekea kuwa kocha aliyecheza mechi nyingi kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya (Mechi 191).

Kipigo hicho kinaacha sintofahamu kubwa kwenye mustakabali wa Ancelotti huko jijini Madrid baada ya pia ushindwa kubeba ubingwa wa La Liga na Ligi Mabingwa Ulaya msimu huu. Madrid ilikuwa ndio mabingwa watetezi wa kombe hilo baada ya kulibeba msimu uliopita kwa mara ya 14.