Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Enzo Fernandez asisitiza kuondoka Chelsea

ENZO Pict

Muktasari:

  • Mazungumzo ya mkataba mpya kati ya Chelsea na wakala wa mchezaji huyo, Javier Pastore, yamegonga mwamba kutokana na Fernandez kutoridhishwa na mshahara.

Kiungo wa Argentina, Enzo Fernandez, anataka kuondoka Chelsea msimu huu wa kiangazi, huku klabu hiyo ikitaka dau la pauni milioni 120 (zaidi ya sh390 bilioni) ili kumwachia.

Real Madrid, Manchester City, na Paris Saint-Germain zinafuatilia kwa karibu hali ya kiungo mwenye umri wa miaka 25. Hali hii inakuja baada ya uhusiano wake na klabu kuzorota, ikiwemo kupewa adhabu ya kufungiwa mechi mbili mapema msimu huu kufuatia vitendo vyake vya ‘kujipendekeza’ kwa Real Madrid wakati wa mapumziko ya mechi za kimataifa mwezi Machi.

Mazungumzo ya mkataba mpya kati ya Chelsea na wakala wa mchezaji huyo, Javier Pastore, yamegonga mwamba kutokana na Fernandez kutoridhishwa na mshahara.

Sera ya Chelsea inategemea bonasi kubwa pale timu inapofuzu michuano ya Ulaya, jambo ambalo hawakulifikia msimu huu. Ingawa kocha mpya wa klabu hiyo, Xabi Alonso, pamoja na wakurugenzi wa ufundi wanataka abaki kwenye mipango ya msimu ujao, huku uongozi wa Stamford Bridge ukikiri kuwa utalazimika kumuuza ikiwa mchezaji huyo atashinikiza kuondoka.

ENZ 01

Mvutano huo ulishika kasi mwezi Machi pale Fernandez alipoikosoa hadharani bodi ya Chelsea kwa kumfuta kazi kocha Enzo Maresca mwezi Januari, kocha ambaye alikuwa anapendwa sana na wachezaji.

Fernandez pia alieleza hadharani hamu yake ya kwenda kuishi jijini Madrid, kauli iliyowaudhi sana viongozi wa juu wa Chelsea.

Hata hivyo, bado kuna mashaka kama Real Madrid, ambayo ndiyo klabu anayoitamani zaidi, itaweza kufikia dau hilo la pauni milioni 120 (Sh422.4 bilioni).

Tangu asajiliwe kwa rekodi ya England ya pauni milioni 106 (Sh373.1 bilioni) Januari 2023 chini ya kocha Graham Potter, maisha ya Fernandez jijini London yamejaa migogoro.

ENZ 02

Tukio kubwa zaidi lilitokea mwaka 2024 alipoweka mtandaoni video iliyomwonyesha yeye na wachezaji wenzake wa Argentina wakiimba wimbo wa kibaguzi dhidi ya wachezaji weusi wa Ufaransa. Kitendo hicho kililaaniwa vikali na mchezaji mwenzake wa Chelsea, Wesley Fofana, aliyeita kitendo hicho kuwa ni ‘ubaguzi wa wazi’, kabla ya Fernandez kuomba radhi kwa timu nzima wakati wa ziara ya maandalizi ya msimu huko Marekani.

Wakati huohuo, kipa wa klabu hiyo Filip Jorgensen naye anatarajiwa kuondoka Chelsea msimu huu baada ya kufanya kikao na wakurugenzi wa ufundi. Jorgensen amekuwa kipa chaguo la pili kwa msimu mzima na ameeleza kutoridhishwa kwake na uhaba wa muda wa kucheza, jambo linalomfanya atafute changamoto mpya.