Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Enzo amalizana na Real Madrid

Muktasari:

  • Kiungo huyo wa Argentina kwa sasa yuko katika Kombe la Dunia akiwa na timu yake ya taifa, lakini taarifa zinaeleza kuwa bado ana nia ya kuondoka Stamford Bridge.

MADRID, England: KIUNGO Enzo Fernandez ameripotiwa kukubaliana masharti binafsi na Real Madrid kuelekea uhamisho unaowezekana kutoka Chelsea FC.

Kiungo huyo wa Argentina kwa sasa yuko katika Kombe la Dunia akiwa na timu yake ya taifa, lakini taarifa zinaeleza kuwa bado ana nia ya kuondoka Stamford Bridge.

Siku chache baada ya kocha Jose Mourinho kuisajilia Real Madrid beki Marc Cucurella, inaelezwa kuwa klabu hiyo imepiga hatua kubwa katika harakati za kumsajili Fernandez.


Makubaliano hadi mwaka 2032

Kwa mujibu wa taarifa hizo, Fernandez mwenye miaka 25 amefikia makubaliano ya awali ya mkataba wa kudumu hadi mwaka 2032 na Real Madrid.

Sasa Madrid wanajiandaa kuwasilisha ofa rasmi kwa Chelsea, ambao wanadaiwa kutaka zaidi ya pauni120 milioni ili kumuuza nyota wao msimu huu wa joto.

Ada hiyo inaweza kuathiriwa pia na uhamisho unaotarajiwa wa Elliot Anderson kwenda Manchester City kwa kiasi kikubwa cha fedha.


Mahusiano na Chelsea yameripotiwa kuzorota

Mshindi wa Kombe la Dunia la 2022 bado ana miaka sita iliyobaki katika mkataba wake wa Chelsea, alioutia saini alipohamia klabuni hapo mwezi Januari 2023.

Hata hivyo, ripoti zinaeleza kuwa kutokubaliana kuhusu kuongeza mkataba wake au kuboresha mshahara wake kutokana na kiwango alichoonyesha kumesababisha mahusiano kati yake na klabu kuwa mabaya.

Baada ya kujiunga na timu ya taifa, Fernandez amekuwa akihusishwa mara kwa mara na Real Madrid, klabu ambayo amewahi kueleza kuwa ni ndoto yake kuichezea.

Madrid ni miongoni mwa klabu chache duniani zenye uwezo wa kifedha wa kugharamia uhamisho wake.


Msimu mzuri Chelsea

Fernandez, ambaye alishinda Kombe la Dunia la Klabu mwaka mmoja uliopita, alifunga mabao 15 katika msimu wa 2025-26 akiwa Chelsea.

Pia aliwahi kuvaa kitambaa cha unahodha katika baadhi ya mechi, lakini sasa inaonekana nafasi yake chini ya kocha mpya Xabi Alonso inaweza kuwa si ya uhakika.

Fernandez aliweka rekodi ya usajili ghali zaidi katika Premier League kwa pauni105 milioni alipowasili Chelsea, kabla ya rekodi hiyo kuvunjwa miezi sita baadaye na mwenzake Moises Caicedo.

Baadhi ya mashabiki pia walitafsiri kitendo chake cha kuwapungia mkono mashabiki wa Chelsea baada ya mechi ya mwisho ya msimu dhidi ya Sunderland AFC kama ishara ya kuaga.

Iwapo Real Madrid watawasilisha ofa inayokidhi mahitaji ya Chelsea, Fernandez anaweza kuwa mmoja wa usajili mkubwa zaidi wa dirisha hili la usajili.