Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

England bila Kane ni majanga

Muktasari:

  • Cole Palmer na Phil Foden walipata nafasi za kucheza kwenye nafasi za mbele wakati England ikikumbana na kipigo cha bao 1-0.

LONDON, ENGLAND: KOCHA wa England, Thomas Tuchel ameshtukia kitu kwenye kikosi hicho kwa kusema washambuliaji waliopewa nafasi katika mchezo wa mwisho wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Japan ambao hakuwepo Harry Kane walipaswa kufanya zaidi.

Cole Palmer na Phil Foden walipata nafasi za kucheza kwenye nafasi za mbele wakati England ikikumbana na kipigo cha bao 1-0.

“Mimi (Tuchel) sio shabiki mkubwa wa kuzungumzia wachezaji mmojammoja, lakini bila shaka ikiwa tunaweka wachezaji wa mashambulizi uwanjani, tunatarajia vitendo vya mashambulizi,” alisema baada ya kuulizwa kuhusu wachezaji hao.

“Tunatarajia ubunifu, mikimbio ya hatari, kupiga mashuti, kusaidia wenzao kufunga na kwa wazi hatukuwa bora vya kutosha kwenye hayo. Hatukuwa katika ubora wetu wa kutengeneza nafasi.”

Kane hakuonekana kuwa tayari kwa mchezo huo baada ya kupata dalili za kuumia katika mazoezi ya Jumatatu.

Tuchel alikiri kuwa itakuwa ngumu kwake kuangalia mechi Ligi Kuu England katika miezi miwili ijayo.

“Wachezaji wetu wamejikita sana kwenye mpira wa klabu, mpira wa Ulaya na wapo kwenye ligi yenye nguvu zaidi,” alisema na kuongeza;

“Harry aliondoka, tulipoteza yeye kama mchezaji na mtu wa kipaumbele. Zipo mechi ambazo tumeshinda bila Harry lakini ni rahisi akiwa pale. Tulipoteza Rice, John Stones ambao ni msingi wa kikosi. Ilituathiri na hiyo ni kawaida. Wanabeba kasi na nguvu kwenye mabega yao.”