Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Elanga amshawishi Isak abaki, asiondoke

ELANGA Pict

Muktasari:

  • Newcastle imefanikiwa kumsajili Elanga kwa ada ya Pauni 55 milioni, ikiamini kwamba winga huyo wa Sweden atamshawishi Isak, ambaye wanacheza timu moja ya taifa pia kubaki kwenye kikosi hicho cha St James’ Park.

NEWCASTLE, ENGLAND: ANTHONY Elanga anapambana kumshawishi straika Alexander Isak asiondoke Newcastle United abaki hapo ili wapige mzigo wakiwa pamoja msimu ujao.

Newcastle imefanikiwa kumsajili Elanga kwa ada ya Pauni 55 milioni, ikiamini kwamba winga huyo wa Sweden atamshawishi Isak, ambaye wanacheza timu moja ya taifa pia kubaki kwenye kikosi hicho cha St James’ Park.

Elanga, 23, alijiunga na Newcastle akitokea Nottingham Forest na anatazamiwa kufanya mambo makubwa akiwa na timu hiyo kwenye ligi msimu ujao.

Isak kwa sasa yupo kwenye rada ya timu ya Liverpool ikihitaji saini yake, licha ya Newcastle kusisitiza kwamba mchezaji huyo hauzwi kwa gharama yoyote, hata kama italipwa Pauni 150 milioni, ambayo wao wanaamini ndiyo thamani yake.

Alipoulizwa kama ana uhakika Isak atabaki, Elanga alisema: “Siku zote kutakuwa na kelele nyingi sana kumhusu, lakini mwisho wa yote, yeye ni mchezaji wa Newcastle United kwa sasa. Kwangu mimi, nitakachofanya ni kuhakikisha anaweka akili yake mazoezini na nitakuwa nikizungumza naye kila siku.

“Alex, kwangu mimi ni straika bora duniani na mtu ambaye si mjuzi tu ndani ya uwanja bali hata nje pia na siku zote amekuwa akikubali ushauri. Siku zote atabaki na kujaribu kunisaidia kama kaka yake. Namkubali sana.”€

Kwenye kikosi cha Newcastle, Elanga anaripotiwa kulipwa mshahara wa Pauni 200,000 kwa wiki na hivyo kuwa mmoja wa wachezaji wanaolipwa vizuri zaidi huko St James’ Park.